KERO Malalamiko kuhusu uongozi wa vyama vya wakulima Tunduru

KERO Malalamiko kuhusu uongozi wa vyama vya wakulima Tunduru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Vyama vya baadhi ya wakulima (AMCOS) katika Wilaya yetu ya Tunduru vinakabiliwa na changamoto ya viongozi wanaohusika na ubadhirifu wa mali za vyama na kutuumiza wakulima.

Baadhi ya viongozi hushirikiana na mawakala na baadhi ya watendaji kuchelewesha malipo, kutosafirisha mazao kwa wakati na kubadilisha ratiba za minada kwa maslahi binafsi.

Hali hiyo imekuwa ikitunyima haki Wakulima kwa muda mrefu, huku hatua za kisheria dhidi ya wahusika zikiwa hazionekani kuchukuliwa.

Tunaomba wizara yenye dhamana kuingilia kati na kuhakikisha usimamizi bora wa vyama vya wakulima ili kulinda maslahi yatu na kuongeza uzalishaji.
 
Back
Top Bottom