KERO Malalamiko kuhusu upendeleo katika kugawa kazi za usimamizi wa mitihani Ifakara

KERO Malalamiko kuhusu upendeleo katika kugawa kazi za usimamizi wa mitihani Ifakara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Valerian1403

New Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Kuna malalamiko kuhusu upendeleo na kutokuwepo kwa usawa katika Idara ya Elimu ya Sekondari ya Halmashauri ya Mji wa Ifakara, hususan katika ugawaji wa kazi maalumu za kusimamia mitihani.

Baadhi ya walimu wanapangiwa siku nyingi za kusimamia mitihani huku wengine wakipangiwa siku chache, licha ya kuwa wanahudumu katika kituo kimoja cha mitihani. Kwa mfano, mwalimu mmoja anaweza kupangiwa siku tano, huku mwingine akipangiwa siku 11.

Hali hii inazua maswali kuhusu vigezo na miongozo inayotumika kugawa kazi hizo. Kwa nini kuwe na tofauti kubwa ya siku za usimamizi wa mitihani kwa walimu walio katika kituo kimoja? Je, ni kwa mujibu wa miongozo ipi inayotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)?

Walimu wanahitaji uwazi na usawa katika ugawaji wa majukumu haya ili kila mmoja apate haki yake bila upendeleo au ubaguzi.

Tunaomba Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) liingilie kati na kuchunguza utaratibu unaotumika katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, ili kubaini kama miongozo inayotolewa inafuatwa na kama kuna ukiukwaji wa taratibu katika ugawaji wa kazi za usimamizi wa mitihani.

Uchunguzi huo pia unaweza kusaidia kubaini changamoto nyingine zilizopo na kuweka utaratibu wa haki, uwazi na uwajibikaji kwa walimu wote.

Tunaomba suala hili lifanyiwe kazi ili kukomesha malalamiko ya upendeleo na kuhakikisha kuwa kazi za usimamizi wa mitihani zinagawiwa kwa kuzingatia vigezo vinavyoeleweka na vinavyokubalika.
 
Back
Top Bottom