A
Anonymous
Guest
Ujumbe huu ufike kwa Afisa Elimu (Wilaya/Mkoa), Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe
Ndugu Afisa Elimu,
Napenda kuwasilisha lalamiko juu ya hali ya uzembe unaoendelea katika baadhi ya shule za msingi zilizopo katika Kata ya Ibumi Wilayani Ludewa. Kumekuwepo na malalamiko ya walimu kutowajibika ipasavyo katika majukumu yao ya kila siku. Wengine hujihusisha na kazi binafsi kama biashara au kilimo, huku wakiacha madarasa bila waalimu.
Kwa masikitiko, hata Afisa Elimu Kata ya Ibumi pia haonekani mara kwa mara kazini, jambo linaloashiria ukosefu wa ufuatiliaji na usimamizi thabiti wa elimu katika kata husika.
Hali hii inadhihirika kwenye matokeo duni ya wanafunzi, kupungua kwa morali ya walimu wachapakazi na kuathiri maendeleo ya elimu kwa ujumla.