Malalamiko ya Kufunga Maduka, Halmashauri ya Kibaha yasema “Wanafunga wenyewe, hatujafunga sisi"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuandika kuwa kuna baadhi ya Maafisa wa Halmashauri wanafunga maduka ya Wafanyabishara kutokana na kuwadai malipo ya Halmashauri hiyo, ufafanuzi umetolewa na Mamlaka husika.

Kumsoma Mwanachama bofya hapa ~ Wafanyabiashara Kibaha tunaishi kama digidigi, tunawakimbia Halmashauri ambao wanafunga maduka yetu

Afisa Mawasiliano wa Halmashauri ya Kibaha Mji, Innocent Byarugaba anaelezea:

Nitoe ufafanuzi kuhusu hoja hiyo ya Mdau, ipo hivi kinachofanywa na Maafisa wa Halmashauri ni kuwapa elimu Wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipia Control Number (Namba ya Malipo) na ili apate namba hiyo lazima mhusika atoe taarifa zake kadhaa.

Namba hiyo inapotolewa Mfanyabiashara anapewa nafasi ya kulipa ndani ya siku tatu hadi saba, anachagua yeye mwenyewe muda wa kulipa ndani ya siku hizo.

Kuanzia Julai 8 hadi Julai 24, 2024, Timu za Mapato ya Halmashauri zimeweza kutoa Namba 971, kati ya hizo Namba 676 zimelipwa, ambazo bado hazijalipwa ni 295.

Hivyo, kinachofanyika ni Timu ya Mapato kwenda kuwaeleza (Wafanyabishara) kuwa namba walizopewa zinaweza kufutika katika karatasi, pia Namba hiyo ikishatolewa lazima ilipwe kwa kuwa kuna suala la ukaguzi.

Timu inapofika kwenye Duka ambalo lina Wafanyabishara wawili, mmoja anabaki anaendelea na biashara, mwingine anaenda Halmashauri kulipa, ikiwa yupo mmoja analazimika kufunga ili aende akalipe na sio kwamba tunawafungia biashara.

Juni ni mwezi wa mwisho kufunga Mwaka wa Fedha, timu ya Halmashauri ya Mji Kibaha iliamua kupita katika Mitaa 73 ndani ya Kata 14 kutoa elimu kuhusu ulipaji wa leseni ikiwa na Wataalam mbalimbali wakiwemo Afisa Biashara, Afisa Masoko, Afisa Viwanda, Bashara na uwekezaji pamoja na Afisa mikopo wa NMB.

Timu hiyo ilikuwa inawafundisha Wafanyabiashara namna ya kukabiliana na soko la ndani na nje na nidhamu ya kutunza fedha kwa kuwa ni wadau wetu ili tunapoanza Mwaka mpya wa Fedha wawe na leseni na mikakati madhubuti ya kulinda biashara zao kwa mujibu wa Sheria.

Kifungu Namba 3 (i) cha Sheria ya Leseni na Biashara ya Mwaka 1972 inaweka katazo kwa Mtu yeyote kufanya biashara kama hana leseni.

Kifungu Namba 8 cha Sheria hiyo kinatoa Mamlaka ya Kutoza Ada ya Leseni, Kifungu Namba 10 kimetoa Adhabu kwa anayefanya Biashara bila Leseni ila sisi hatukutoa adhabu.

Kifungu cha Namba 6, Kifungu Kidogo (I) E cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mtaa ya Mwaka 1982, Namba 9 kinasema Ada zote za leseni ni chanzo cha mapato kwa Halmashauri ya Mji.

Nawasii Wafanyabiashara walipe Leseni kwa kuwa zinasaidia maendeleo ya Nchi yanayofanywa na Serikali.
 
"Kwamba wanafunga wenyewe na pia kulalamika wenyewe!"

Si hawa ndugu wakawape ufafanuzi huo ndege?
 
kuwapa elimu Wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipia Control Number (Namba ya Malipo) na ili apate namba hiyo lazima mhusika atoe taarifa zake kadhaa.

Naomba ufananuzi kidogo: una maanisha kila mfanya booashara anwe na control number yake? au kuna mlaipo flani wanatakiwa kulipia kupitia control number? na ni malipo ya nini?
 
Back
Top Bottom