Malalamiko ya tozo

Raphael Thedomiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2019
Posts
442
Reaction score
729
Serikali ina wajibu na inapaswa kubeba jukumu la kuyaondoa malalamiko yetu wananchi wao dhidi yao.

Haipaswi kuyafumbia macho na kuziba masikio wasiyasikie, kwani yanaweza hata kuhatarisha utulivu na ustawi wetu wa kijamii.

Uwazi kadri iwezekanavyo katika makusanyo ya tozo zetu inaweza kusaidia.

Tutozwe tozo ambazo tunafahamu katika uwazi wote kuwa ni kwa ajili ya kufanyia nini, na tuone kweli kwamba lengo hilo linasimamiwa na kutekelezwa katika uwazi wote unaowezekana.

Hivyo tutachanga kwa furaha na kwa mshikamano.
 

Serikali kiziwi inasikia je mkuu? Kwa kuwabembeleza, au kulia lia kama hivi?

Waliojinadi kuwa Serikali Sikivu wamethibika kuwa Viziwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…