mzalendoalltz
JF-Expert Member
- Mar 25, 2015
- 828
- 709
Wananchi wengi wanalalamika hasa suala la upendeleo wa wazi unaoonyeshwa na wasimamizi wa eneo tengwa la barabara yaani (Road reserve) tunaona serikali inafanya jitahada za kuwaondoa wavamizi sawa ila idara hii imekuwa sugu kwa Rushwa maana kuna watu wengi wapo na hawaondolewi na wamekaa miaka na miaka, wengine tunaondolewa kwa nguvu kubwa na wengine tupo nje lakini wakija kupima wanatupa notice za kubomoa na ukienda wanakudai pesa ili wakusamehe.
Tunamuomba Mh Rais Samia kupitia kwa waziri Mbarawa afanye uchunguzi wa kina. ajiridhishe ili awawajibishe wahusika na zaidi aangalie idara yake pale Tanroads Dar (Meneja Mkoa) eidha anaesamia idara hiyo ndiye anamuangusha kwa kutokuwa makini na usimamizi. Tunawakilisha Kazi iendelee upendeleo wa kirushwa ufutwe kabisa.
Tunachotaka sisi ni haki kama mmesema eneo ni la Serikali bas asitumie mtu yeyote na kama litatumika tupewe hiyo haki wote.