A
Anonymous
Guest
Sisi walimu tuliomaliza mafunzo ya ualimu ngazi ya Astashahada miaka iliyopita, baadaye tukaamua kujiendeleza hadi ngazi ya Shahada, tunaomba ufafanuzi kuhusu changamoto inayotukabili katika ajira.
Tulishiriki usaili kwa kutumia vyeti vyetu vya Astashahada, lakini wakati wa upangaji wa ajira tunaambiwa kuwa tumekuwa overqualified kwa sababu tayari tuna Shahada.
Tunajiuliza, je, ni kweli mtu anapokuwa na sifa za juu zaidi hawezi kuajiriwa katika nafasi ambayo ana sifa zake za awali? Wakati tunapojiendeleza kielimu, hatukupewa taarifa kwamba kufanya hivyo kungetufanya tusistahili tena kuomba nafasi za ajira zinazolingana na vyeti vyetu vya awali.
Tunaomba mamlaka husika zilichunguze suala hili kwa haki na kutoa ufafanuzi kwa waombaji. Ikiwa tulitimiza vigezo vya nafasi husika, tukafanya usaili na kufaulu, tunaomba tupewe nafasi ya kuajiriwa kama walivyopewa waombaji wengine.
Tuliingia darasani, tukasoma na kufuzu kwa lengo la kupata ajira na kujenga maisha yetu. Kujiendeleza kielimu hakupaswi kuwa sababu ya kutunyima fursa tuliyokuwa na sifa nayo, hasa kama hakukuwa na taarifa ya awali kwamba kuendelea na Shahada kungetufanya tusistahili kuomba nafasi hizo.
Tunaomba haki itendeke na suala hili lifanyiwe kazi ili walimu tuliokidhi vigezo na kufaulu usaili tupatiwe nafasi ya ajira.