KERO Malalamiko ya watumishi wa Idara ya Elimu ya Sekondari Halmashauri ya Tarime Vijijini kuhusu kutolipwa stahiki zetu

KERO Malalamiko ya watumishi wa Idara ya Elimu ya Sekondari Halmashauri ya Tarime Vijijini kuhusu kutolipwa stahiki zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Watumishi wa Halmashauri ya Tarime Vijijini, Idara ya Elimu ya Sekondari, tunalalamikia kutolipwa stahiki zetu za likizo ya malipo licha ya kudai kwa muda mrefu.

Kila tunapofuatilia tunaelezwa kuwa fedha zinazotolewa na Serikali hazitoshi, jambo linalotushangaza kwa kuwa watumishi wa Idara ya Elimu ya Msingi wanalipwa kwa wakati na kwa kiwango stahiki.

Kwa upande wetu, hata pale ambapo baadhi hulipwa, kiasi kinachotolewa huwa kidogo kuliko stahiki inayopaswa kulipwa. Mfano, mtumishi anayestahili kulipwa kulingana na umbali na hali ya familia kiasi cha shilingi 500,000 anaweza kupewa shilingi 100,000 bila maelezo ya msingi.

Aidha, bado tunadai malipo ya mishahara ya kwanza tangu tulipoajiriwa, lakini hadi leo hatujalipwa. Tunapofika kwenye ofisi husika kwa ajili ya kupata maelekezo na msaada, tunaishia kuzungushwa bila kupata suluhisho.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuhakikisha tunalipwa stahiki zetu kwa wakati.
 
Kero yangu ni Idara ya Elimu Sekondari - Halmashauri ya Tarime, wafanyakazi wanaenda likizo wanacheleweshewa malipo yao ya nauli mfano walioenda Desemba 2025 hawajalipwa mpaka leo wakati Idara ya Msingi wameshalipwa mpaka June 2026.
 
Back
Top Bottom