Malaria kujirudiarudia nini sababu?

Pole sana mkuu.
Tunakitu tunaita Congenital Malaria/malaria sugu/malaria ya kuzaliwa nayo ndo maana mama mjamzito anapewa Dawa za Sulphur Sp ili kumkinga kiumbe aliyeko tumboni.

Twende kwenye mada yako je unaishi ukanda wenye Malaria kwa wingi mfano Tanga,Dar,Morogoro au pwani(Endemic area)?

Je unalala kwenye Chandarua chenye dawa,vipi mazingira ya nyumba yako kuna madimbwi,mito,ziwa,majani marefu karibu au hata miti miti?

Je madirisha yana wiremesh,je wakati wa usiku unavaa nguo ndefu au unashinda na kaptula?

Je unatumia dawa ulizoandikiwa na dr au unanunua kwenye maduka ya dawa na je umeshawahi kuangalia expiry ya dawa unazotumia?

Je unatibiwa na Dr au?manake kama ni dr anaweza kwenda kwenye Second line ya dawa kama ugonjwa umekua sugu.

Pia nimeona kwamba unatumia Malafin ila kwa uelewa wangu mdogo sidhani kama Malafin ipo kwenye Guideline ya dawa za malaria kutoka wizara ya afya.

Mpaka mara ya mwisho nasoma tunatumia Mseto/Alu As the first line drugs for uncomplicated malaria na Quinine kama Second line for Severe Malaria eventhough kuna Artesunate injection na Arthemether inj nazo zinaweza kutumika kwa Malaria kama yako iyo.

Ushauri narudia tena ushauri Nenda hospitalini kamweleze Dr na sio kwenda maabara na kupima na kwenda pharmacy kununua dawa.

Pia Malaria yaweza sababisha kifua respiratory distress ni kati ya complication za malaria.

Narudia tena nenda hospitalin ndugu achana na zile nami nilitumia dawa iyo ikanisaidia
 
Mmmmh msisingizie O+ mbona wengine hatuugui si malaria wala kikohozi
Mm mwenyewe ni group 0+,kwangu malaria ni makao makuu,haishi miezi miwili naumwa malaria mpaka ilibidi nipime vipimo vikubwa holaaah,ndipo dr aliponiambia nipime group la damu ikawa +ve nikaambiwa ni sifa mojawapo ya kuumwa malaria kwa wenye group hili.
 
Asante mkuu yaan umetoa ushaur waki medical kabisa nitafuata ushauri wako.
 
Binafsi,nilikuwa nasumbuliwa sana kila baada ya wiki mbili nilikuwa natumai dose,lakini nilipata ushauri kwa daktari moja Na kutumia dawa aina ya "Atequin ya uswis". Nilitumia dose moja kila mwezi kwa miezi mitatau ikiwa ni sawa Na dose Tatu. Tangu hapo sijapata malaria Na huu ni mwaka Wa NNE naelekea Wa tano bila malaria.
 
Mmmmh [emoji102] [emoji101] mimi siumwigi huo ugonjwa na situmii neti
 
Nilikuwa naishi shinyanga lakini nilikuwa naugua hivyo hivyo saizi nipo katavi lakin kila baada ya miezi mitatu au miwili naugua kiukwel huwa situmii neti kipindi nasoma ndio nilikuwa natumia lakin nilikuwa naugua tu hata nikitumia. Let me know are you MD or Nurse or AMO?
 
Mkuu hiyo dawa inapatikana maduka yote?
 
Kapime Tb ya mifupa haraka sana
 
Punguza presha, tb ya mifupa kwani una dalili zozote za kifua kikuu?
Hapana sina na nmesha pima nikaambiwa sina nmesha piga na x ray ilikuangalia kama kwenye mapafu kunatatzo nkaambiwa sina.
 
Fanya hivi ukiumwa malaria tena usitumie ALU tumia dose ya quinine na umalize dose kabisa..
 
Mara ya mwisho kupima ngoma ilikuwa lini?......Kwa sababu inawezekana ikawa ni ngoma!
 
Hapana sina na nmesha pima nikaambiwa sina nmesha piga na x ray ilikuangalia kama kwenye mapafu kunatatzo nkaambiwa sina.
Amini hiyo ni malaria ya kawaida tu. Nimesumbuliwa sana na malaria tangu niko na 20 hadi sasa niko na 30+ ilikuwa kila mwezi lazima niugue malaria, lakini sahivi niko fresh, ikiwezekana nenda kwa ma specialist au ufanyiwe kipimo cha blood culture ili kujua ni nini kinachokusibu.
 
Maambukizi ya malaria huchukua siku 14 mpaka dalili za ugonjwa jujitokeza, kuna uwezekano mkubwa kuwa unapata maambukizi mapya.

Kula vizuri nya na mboga za majani pia fanya mazoezi kuimarisha immune system yako
Mshauri mwenzio apime HIV pia!!
 
Maambukizi ya malaria huchukua siku 14 mpaka dalili za ugonjwa jujitokeza, kuna uwezekano mkubwa kuwa unapata maambukizi mapya.

Kula vizuri nya na mboga za majani pia fanya mazoezi kuimarisha immune system yako
Kwa kuongezea tu,take preventive measures. Tumia net ulalapo,paka repellent,safisha mazalia ya mbu. Huwa hakuna malaria sugu ila kuna mazalia sugu ya mbu.
 
Kwani wewe kunadawa uliyo itumia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…