Malaria kujirudiarudia nini sababu?

Mwaka jana na hili tatizo limenianza kitambo mno.
Huwa una tabia ya kufanya kati ya haya?

1.Kutokumaliza dozi
2.Kutokutumia dozi ipasavyo(Kuruka mda wa kula dawa mfano unatakiwa kumeza vidonge kila baada ya masaa nane ila kwa bahati mbaya unatakiwa kuamka saa nane ya usiku ili ule vidonge ila kwa bahati mbaya ukapitiliza bila kula huo mda)
3.Kula dawa za malaria pale unapohisi kuumwa bila kwenda kupima kwanza malaria kwenye kituo cha Afya
 
Kwani wewe kunadawa uliyo itumia?
Nilijitibu kwa kutumia chakula tu, kula msosi rich in milo yote, matunda kwa wingi, then mi situmii pombe. Hivyo tangu mwezi wa nane hadi sasa naona mafanikio.
 
Nilijitibu kwa kutumia chakula tu, kula msosi rich in milo yote, matunda kwa wingi, then mi situmii pombe. Hivyo tangu mwezi wa nane hadi sasa naona mafanikio.
Bila kusahaukufanya mazoezi walau nusu saa kwa siku, muda wa jioni huws napendelea kuvaa t sheti ya mikono mirefu na kuvaa soksi miguuni, kwa vile napendelea sana kuwepo nje ya nyumba kwa muda huo.
 
Zamani ndio nilikuwa na tabia hizo zote maana nilikuwa simalizi dozi kabisaaa kutokana na hali kwetu ilikuwa duni sana hivyo kupata hela ya kununulia dawa dozi nzima ilikuwa ni ngum mno ndugu nadhan ndio ilijenga kitu kinacho itwa contraindication.
 
jaribu pia kuishi mazingira ya baridi kama mbeya na mafinga....wakati mwingine mazingira huchangia
 
Zamani ndio nilikuwa na tabia hizo zote maana nilikuwa simalizi dozi kabisaaa kutokana na hali kwetu ilikuwa duni sana hivyo kupata hela ya kununulia dawa dozi nzima ilikuwa ni ngum mno ndugu nadhan ndio ilijenga kitu kinacho itwa contraindication.
Kama una moja ya tabia hizo au zote basi vimelea vya malaria huwa vinakuwa sugu kwa dawa ambazo unakuwa unatumia!!
 
Kwani huwa una meza au una andkiwaga dawa gan ya malaria mara kwa mara!? Tuanze hapo!
 
Kwani huwa una meza au una andkiwaga dawa gan ya malaria mara kwa mara!? Tuanze hapo!
Mara nying huwa naenda kwenye vidispensary nikipimwa wakinigundua nna malaria naambiwa huwa unatumia dawa gan ya malaria? Najibu Malafin ndio naandikiwa hiyohiyo.
 
Mara nying huwa naenda kwenye vidispensary nikipimwa wakinigundua nna malaria naambiwa huwa unatumia dawa gan ya malaria? Najibu Malafin ndio naandikiwa hiyohiyo.
Sasa tatizo ndo lina anzia hapo izo malafin sijui Orodar hizo ziko kwnye kundi la SP hizo siyo sawa za malaria bali ni prophylasis( kinga ya malaria) na ndio maana clinic huwa tuna wapa wajawazito ili kuzuia malaria kwao.
 
Em nishaur sasa hapo mkuu kwahyo nije nihamie kwenye second line? Maana nikipimwa wanakuta ni uncomplicated sio complicated malaria; au ni first line gan itakua nzur?
 
Maana doctor mwenyewe wavidispensary ananipa hapo ndo sielewi kidogo.
 
Kiukwel hili tatzo lakuugua mara kwa mara ninalo tangu nipo namiaka 7 mpaka sasa ninamiaka 24 linanisumbua tu nikienda kupima naambiwa ni malaria natumia malafin baada ya miez mitatu hivyohivyo tu HIV nimeshapima kabisaaa.
Weraaaa wewe ulikuwa kama Mimi aise ,ila tatizo lako no dogo sanaa ni kwamba hiyo dawa haiko countability na body immunity yako.Luna dawa moja za marelia za nje kutoka ufaransa na ubergiji hizo dawa in nadra utazikuta kwenye maduka makubwa tu bei inaweza fika hats 35tsh less than 30 usinunue itakuwa fake ,piga hiyo kitu mkataba miaka 2 hadi 3 unadunda tu.ukishindwa weka mseto uone mwisho wa matatizo mwisho usidharau kulalia net.
 
Dawa huwa zinagoma. Kuna teenager hapa nyumbani ni group O+ anaumwa sana malaria kuna wakati hata hiyo Artequin ya Switzerland imegoma. Tulipoona hakaponi ikabidi kapime ngoma. Hana. Nakushauri uanze natural remedies. Kunywa punje 6 za vitunguu swaumu asubuhi kabla ya kula chochote. Kunywa Maji ukiweza lita 2-3 kwa siku. Usiku kunywa tena vitunguu. Wiki 3.Tahadhari!!! Hakikisha huna BP ya kushuka. Pia nunua "Black Seed Oil" uwe unakunywa kijiko kimoja cha chai asbh, mchana na jioni. Asali ongezea hapo. Kula sana matunda.
 
Em nishaur sasa hapo mkuu kwahyo nije nihamie kwenye second line? Maana nikipimwa wanakuta ni uncomplicated sio complicated malaria; au ni first line gan itakua nzur?
Mseto wa ALU una ufanisi mkubwa!! Tatizo ivyo vi mahabara na vi dispnsary mtaani wako ki maslahi zaidi huwez enda wasi kwambie hauna Malaria.. jitahd uwe unakwenda hosptal za serikal haswa uwe unapimwa kwa MRDT japokuwa microscope ni gold standard lakn wrong result ni nyingi na mtu kudanganya ni rahisi.

NOTE: izo ant Malaria nazo zina sideffct na zina chosha ini ivyo kumeza dawa ovyo hutakuwa hauna tofauti na mtumiaji wa ARvs
 
Dah! Nilisha enda hadi Tiens hao wamasuala ya herbal et wanakifaa ambacho unakishika alafu wanakwambia kinapima magonjwa yote mwilini wakanipima bhana eti wananpa majibu mara kwenye mapafu kunavumbi mara oooooh huna nguvu zakiume dah! Nkashangaa kuja kwenye dawa zao Laki mbili na nusu nikakimbia mbio za hatar.
 
Siunajua tena gvt hospitals folen? Em ngoja nije tu nijarb kuwaambia watumie MRDT maana duh! Shida kweli kweli.
 
Umewahi kunywa Oroda? Unakunywa dozi mbili. Ukinywa kwa mfano leo tarehe 14/12/17 unairudia tena same date January 18. Kuna mtu imemsaidia amepumzika miezi 6 bila kuumwa baada ya kuwa anaumwa miaka 4 bila kupona.
 
Unatumia kipimo kipi cha malaria? Hakikisha unatumia kile cha kuangalia kwa microscope, vile vipimo vya kubadilika rangi havifanyi kazi sawa.
Unatumia dawa gani na unatumia hadi dozi inaisha? Malaria mara nyingi haiondoki mwilini ila inajificha hasa kwenye liver ila kila miezi mitatu nadhani kuna ishu nyingine, labda unatumia dawa sio nzuri au haumalizi dozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…