Malaria ya ubongo(Cerebral Malaria)

Malaria ya ubongo(Cerebral Malaria)

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
4,118
Reaction score
1,970
Ninaye mdogo wangu ambaye anakaribia kumchumbia rafiki yake wa kike.Moja ya vitu ambavyo bwana mdogo alivifanya,ilikuwa ni kumuuliza msichana wake kama anayo magonjwa yoyote ya hatari.Msichana bila hiyana akamweleza ukweli kuwa huwa ana malaria ambayo huwa inapanda kichwani(cerebral malaria)na akamweleza kuwa hilo tatizo huwa linajitokeza walau mara moja kila mwaka.

Sasa bandugu nauliza,kuna madhara makubwa kiasi gani ambayo yanaweza kuletwa na malaria hii na hatimaye kuwa kikwazo katika ndoa ya wawili hawa?Kuna matibabu ya kukomesha tatizo hili au inawezekana ni ugonjwa wa kurithi?(ingawa binti alimwambia dogo kuwa hakuna mtu mwenye tatizo hilo kwenye familia yao).

Je,zipo njia ambazo mdogo mtu aweza kuzitumia kulivumilia tatizo hili na kuendelea na hatua za kuchumbia,je kuna madhara gani kindoa,na kwa watoto watakaozaliwa?.


Waiting wadau!
 
Malaria ya aina hiyo yaweza mpata mtu yoyote yule,si kwamba ni ugonjwa wa aina tofauti ni malaria tu ambayo huwa kali sana,yaani malaria strains wanakuwa wanashambulia cells kwenye celebral part of the brain, humfanya mtu ,kupata joto kali,kichefuchefu,kizunguzungu,kutapika na homa kali.nk,kinga ni kujikinga na mbu waenezao malaria,kuwa na utamaduni wa kufanya blood checkup walau kila mwezi.
 
Isaac kamaliza kila kitu, issue hapa pale anapoanza kujisikia kuumwa aende hospital mapema, na pia ajikinge na mbu.
Jambo jingine fuatilia history ya huyo dada kwa watu wa karibu yake au majirani wengine huwa si malaria per say ila inakuwa kifafa au kichaa sasa haya si mazuri kwa wanandoa coz haya magonjwa yana run in families, so asije ambukiza uzao wake. Still do some investigations
 
Huo ni uongo mkubwa!!!

Malaria kali/Hatari(Cerebral Malaria) ni aina ya malaria ambayo ni:
1/Mtu yoyote anaweza kuupata kwa kung'atwa na mbu mwenye vimelea.

2/Uua kwa haraka kama ukimpata mtu(Hauwezi kukaa zaidi ya wiki 3, ama upone au ufe)

3/Sio ugonjwa wa kudumu(Chronic)

4/Sio ugonjwa wa kujirudiarudia(Recurrent)

5/Mtu akiupata ama apone(Kama atatibiwa haraka na vizuri) ama afe wakati ule ule akiwa anaumwa.

6/Ni ugonjwa wa kuambukiza(Kwa kung'atwa na mbu), unazuilika na unatibika 100%

7/Dalili kuu zake ni Homa kali Maumivu makali ya kichwa na kuchanganyikiwa au kutojitambua kabisa.

*Huyu dada kuna uwezekano akawa anaumwa aina fulani ya kifafa(temporal-occipital seizure disorder) au aina fulani ya ugonjwa wa kiakili(Mania) nk.
But sidhani kama ni Cerebral Malaria kabisa.

*Kifupi Cerebral malaria sio issue kwenye mahusiano but ni ugonjwa hatari unaoua sana tena kwa haraka kama hautatibiwa vema na kwa wakati ule ule na mtu hawezi kuendelea kuishi nao mwilini unless afe au apone.

*Hivyo dogo anabidi achunguze zaidi mambo mengine maana kuna kitu fulani kimejificha hapo ama kwa makusudi au kwa kutokujua.

Ngoja tusubiri wataalam wa afya hapa JF watujuze zaidi.....
 
Back
Top Bottom