mayenga
JF-Expert Member
- Sep 6, 2009
- 4,118
- 1,970
Ninaye mdogo wangu ambaye anakaribia kumchumbia rafiki yake wa kike.Moja ya vitu ambavyo bwana mdogo alivifanya,ilikuwa ni kumuuliza msichana wake kama anayo magonjwa yoyote ya hatari.Msichana bila hiyana akamweleza ukweli kuwa huwa ana malaria ambayo huwa inapanda kichwani(cerebral malaria)na akamweleza kuwa hilo tatizo huwa linajitokeza walau mara moja kila mwaka.
Sasa bandugu nauliza,kuna madhara makubwa kiasi gani ambayo yanaweza kuletwa na malaria hii na hatimaye kuwa kikwazo katika ndoa ya wawili hawa?Kuna matibabu ya kukomesha tatizo hili au inawezekana ni ugonjwa wa kurithi?(ingawa binti alimwambia dogo kuwa hakuna mtu mwenye tatizo hilo kwenye familia yao).
Je,zipo njia ambazo mdogo mtu aweza kuzitumia kulivumilia tatizo hili na kuendelea na hatua za kuchumbia,je kuna madhara gani kindoa,na kwa watoto watakaozaliwa?.
Waiting wadau!