Malawi: Akamatwa akichomoa mipira ya drip za wagonjwa ili wafe auze masanduku

Malawi: Akamatwa akichomoa mipira ya drip za wagonjwa ili wafe auze masanduku

Akilihuru

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2022
Posts
1,512
Reaction score
2,980
Za mchana wakuu,

Hii imetokea huko nchini Malawi, jamaa mmoja muuza masanduku anaeishi karibu na hospital fulan ya umma aliingia katika hospital hiyo kinyemela na kuanza kuchomoa mipira ya drip walizowekewa wagonjwa wa kipindupindu ili wafe na yeye apate nafasi ya kuuza masanduku yake.

Alivyohojiwa alikiri kufanya kitendo hicho, lakini alijitetea kwamba alifanya hivyo kwa lengo la kujitafuta riziki baada ya kukaa muda mrefu bila kuuza masanduku hayo na pia ukali wa maisha uliyopo nchini humo umechangia.

Dah dunia imegeuka jahannam, watu hawana utu kabisa.
===


Jamaa mmoja kutoka Nchini Malawi katika Jiji La Blantyre amenusurika kifo mara baada ya kupata kipigo kutoka kwa Raia wenye hasira kali mara baada ya kuingia katika wodi ya wagonjwa wa kipindu pindu huko Limbe kisha kuchomoa drip ili wagonjwa wafariki na yeye auze majenezeza.

Mara baada ya kuhojiwa jamaa huyo akajibu kuwa ugumu wa biashara hiyo umesababisha yeye kufanya jambo hilo lililo acha hoi watu wengi waliokuwa eneo hilo.

Chanzo: VOT Media
 
Unakuta mtu kama huyo anaenda kanisani/msikitini kumwomba M/Mungu ambariki katika biashara yake ya majeneza.Dunia dah
 
Chai ya rangi na tangawizi hiyo. Taarifa isiyotaja muda na mahali ni feki!
 
Sikumbuki ni nani aliwahi kuleta uzi wa jamaa aliekua anaua wagonjwa ili apate tenda ya kuwachimbia makaburi.

Kuna baadhi ya kazi zinafanya watu wawe na roho za kikatili, wakiwemo pia wachinja mifugo kama mikubwa kama mbuzi, ng'ombe n.k , wauza bucha
 
Kwani huyo ana tofauti gani na mwanasiasa anayenunua gari la 600M ama anasaini mktaba wa software ya India inayofuatilia umeme kukatika badala ya kujenga dispensary ama kuongeza vifaa Bora ili mama wajawazito wapate huduma nzuri na wagonjwa wengine na sio lazima kukimbizwa na ambulance mpaka mkoa wa mbali wanakufa.

Ama walimu wazuri mazingira mazuri kwao pia na vitabu vya kutosha kwa watoto baadaye watt wanafeli tunapata vibaka na Malaya, watt wetu wanafariki kwa magonjwa ya zinaa na wengine wanauwa kwa wizi ama kula dawa Mana hawakupata elimu nzuri na sahihi. Ama nyie mnacheki mauaji indirect
 
Chai ya rangi na tangawizi hiyo. Taarifa isiyotaja muda na mahali ni feki!
Nami niliisikia jana hii taarifa ni zambia kama sijakosea na wagonjwa wenyewe walikua wa kipindupindu kwa hyo kwa kuchomoa zile dripu za maji nahisi kama wakati wao umefika wangekufa wengi, mtihani sana
 
Wapo watakaosema anatafuta ridhiki maana ndio msemo wa siku hizi kwa kila anayekwenda kinyume
 
Nami niliisikia jana hii taarifa ni zambia kama sijakosea na wagonjwa wenyewe walikua wa kipindupindu kwa hyo kwa kuchomoa zile dripu za maji nahisi kama wakati wao umefika wangekufa wengi, mtihani sana
Hapana ni Malawi mkuu. Ila shukran kwa kunisaidia kumuaminisha huyo mbishaji.
 
Back
Top Bottom