Hii imetokea huko nchini Malawi, jamaa mmoja muuza masanduku anaeishi karibu na hospital fulan ya umma aliingia katika hospital hiyo kinyemela na kuanza kuchomoa mipira ya drip walizowekewa wagonjwa wa kipindupindu ili wafe na yeye apate nafasi ya kuuza masanduku yake.
Alivyohojiwa alikiri kufanya kitendo hicho, lakini alijitetea kwamba alifanya hivyo kwa lengo la kujitafuta riziki baada ya kukaa muda mrefu bila kuuza masanduku hayo na pia ukali wa maisha uliyopo nchini humo umechangia.
Dah dunia imegeuka jahannam, watu hawana utu kabisa.
===
Your browser is not able to display this video.
Jamaa mmoja kutoka Nchini Malawi katika Jiji La Blantyre amenusurika kifo mara baada ya kupata kipigo kutoka kwa Raia wenye hasira kali mara baada ya kuingia katika wodi ya wagonjwa wa kipindu pindu huko Limbe kisha kuchomoa drip ili wagonjwa wafariki na yeye auze majenezeza.
Mara baada ya kuhojiwa jamaa huyo akajibu kuwa ugumu wa biashara hiyo umesababisha yeye kufanya jambo hilo lililo acha hoi watu wengi waliokuwa eneo hilo.
Kwani huyo ana tofauti gani na mwanasiasa anayenunua gari la 600M ama anasaini mktaba wa software ya India inayofuatilia umeme kukatika badala ya kujenga dispensary ama kuongeza vifaa Bora ili mama wajawazito wapate huduma nzuri na wagonjwa wengine na sio lazima kukimbizwa na ambulance mpaka mkoa wa mbali wanakufa.
Ama walimu wazuri mazingira mazuri kwao pia na vitabu vya kutosha kwa watoto baadaye watt wanafeli tunapata vibaka na Malaya, watt wetu wanafariki kwa magonjwa ya zinaa na wengine wanauwa kwa wizi ama kula dawa Mana hawakupata elimu nzuri na sahihi. Ama nyie mnacheki mauaji indirect
Nami niliisikia jana hii taarifa ni zambia kama sijakosea na wagonjwa wenyewe walikua wa kipindupindu kwa hyo kwa kuchomoa zile dripu za maji nahisi kama wakati wao umefika wangekufa wengi, mtihani sana
Nami niliisikia jana hii taarifa ni zambia kama sijakosea na wagonjwa wenyewe walikua wa kipindupindu kwa hyo kwa kuchomoa zile dripu za maji nahisi kama wakati wao umefika wangekufa wengi, mtihani sana