Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 8,105
- 20,307
Siku moja kabla ya kifo cha billionea mtata Wicknell Chivayo iliripotiwa kumatwa kwa shehena kubwa ya silaha haramu zikiwa zinasafirishwa kutoka Zimbabwe kuelekea Sudan kusini kupitia nchi ya Malawi hali iliyopelekea mkuu wa majeshi wa nchi hiyo kukamatwa kwa uchunguzi zaidi.
Hali inaelekea kuwa mbaya zaidi kwa mkuu huyo wa majeshi kwani baada ya kifo cha Wicknell Chivayo ushahidi zaidi umezidi kutolewa kuhusu biashara haramu alizokuwa akifanya na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Jenerali Phiri, ambaye aliongoza jeshi la Malawi kuanzia Julai 2023 hadi Oktoba 2025, anakabiliwa na mashtaka mbalimbali mazito ikiwemo:
Kama tunavyojua, tangu mwezi Aprili 2023, nchi ya Sudan imeingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Jeshi la Serikali (SAF) na Kikosi cha Migambo cha Rapid Support Forces (RSF).
Mgogoro huo umekuwa ukipokea silaha kupitia njia mbalimbali za panya barani Afrika, na sasa inagundulika kuwa maafisa wa ngazi za juu za kijeshi katika ukanda wetu wanahusika kufanya biashara na makundi hayo!
Chanzo: Malawi ex-army chief arrested following allegations over Sudan arms

- Matumizi mabaya ya madaraka (Abuse of Office)
- Kujihusisha na biashara au umiliki wa mali zinazohusishwa na vitendo vya Ugaidi (Dealing in terrorist property)