Malawi: Rais Chakwera akosolewa kwa kuteua ndugu kwenye Baraza la Mawaziri

Malawi: Rais Chakwera akosolewa kwa kuteua ndugu kwenye Baraza la Mawaziri

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Rais mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amekosolewa kwa kuteua Baraza la Mawaziri linalojumuisha Mtu na Mke wake pamoja na watu wengine ambao ni ndugu

Sidik Mia, ambaye ni Mgombea mwenza wa Rais huyo katika Uchaguzi wa mwaka 2019 amechaguliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi huku mke wake, Abida Mia akiwa Naibu Waziri wa Ardhi

Kenny Kandodo ni Waziri mpya wa Kazi huku dada yake, Khumbize Kandodo akiwa ni Waziri mpya wa Afya. Mfanyabiashara Gospel Kazako amekuwa Waziri wa Habari huku Shemeji yake, Agnes Nkusa Nkhoma akiwa Naibu Waziri wa Kilimo

Baadhi ya Wakosoaji wameshangazwa na Baraza hilo kwani Rais Chakwera amefanya kile ambacho aliwahi kumkosoa nacho aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kuhusu upendeleo na kuteua watu kutoka mkoani kwake

Wameongeza kuwa zaidi ya asilimia 79 ya Baraza jipya la Mawaziri wanatokea Mkoa wa Kati ambapo Rais Chakwera anawafuasi wengi
 
Aisee anagawa tu keki ya taifa --- bila shaka hao ndio waliokuwa wafadhili wake wakati wa kampeni so anarejesha kile walicho mkopesha
 
Ame anza kujikuta nabii[emoji28][emoji28]
 
Ni watu wake wa karibu ambao anaamini hawatamuangusha kwenye utendaji kazi. Kwa upande mwingine, inawezekana kwa namna moja au nyingine walimuwezesha kufikia hapo alipo. Ameona siyo mbaya kurudisha fadhila!
 
Nadhani ni rahisi kufanya kazi na mtu unayemuamini, ila binafsi bado simuamini Chakwera.
 
Kavurunda huyu kuchagua ndugu kama kaka na dada. Pamoja na hao ndugu yeye binafsi hawamuhusu lakini KAVURUNDA sana.
 
Pia kampa shavu la uwaziri mtoto wa Joyce banda raisi aliepita. Hivyo tayari kuna double standards hataweza kushughulikia ufisadi wa huyo mama maana nae alimuunga mkono sana kwenye kampeni.
 
Kuna Mtu Mmoja aliwahi kuniambia Mzukulu kuwa Waafrika wengi ni Watu wa Kupenda sana Mabadiliko na Ujio wa Vyama vingi katika Kushika Dola za nchi zetu hizi ila hapo hapo Waafrika tumesahau kwamba tabia zetu za Kiafrika zinafanana hata kama tutakuwa tunampenda na Kumuamini Mtu fulani kutokea upande tuupendao na kuuchukia ule atokao.

Ni kwamba katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ambayo pia imepelekea hata Wananchi wa Malawi ambao walimpigia Kura sasa Kujutia Kumuweka Madarakani Rais Mteule wa Malawi Mwinjilisti Lazarus Chakwera ameanza Mazingaombwe yake na Upuuzi wake kwa Kuteua Baraza la Mawaziri ambalo humo humo lina Ndugu na Mashemeji ikiashiria anatanguliza Undugu Serikalini.

Kwa kuanzia tu ameteua Waziri wa Kazi na wa Afya ambao wote Wawili ni Ndugu moja kwa Baba na Mama. Kuona hiyo haitoshi Kateua Waziri wake mpya wa Habari ambaye kumbe nae ni Shemeji wa Naibu Waziri wa Kilimo. Na kwa Kumalizia Upuuzi wake Rais huyu Kateua tena Waziri wa Usafirishaji ambaye tena ni Mume wa Naibu Waziri wa Ardhi.

Ndiyo maana kuna muda Mzukulu huwa nasema ni kheri tu nchi za Afrika ziendelee Kuongozwa na Marais Wakongwe kuliko Wapuuzi kama hawa.

Kwa anayetaka Taarifa hii Kamili ipo katika Gazeti la Mtandao la The Citizen.
 
Taarifa imezagaa dunia nzima af unatuelekeza tukasome the citizen...
 
Taarifa imezagaa dunia nzima af unatuelekeza tukasome the citizen...

Nimeipata kutokea Gazeti hilo la The Citizen hivyo ningekuwa ni Mpumbavu kama Wewe niseme nimeitolea huko Kwingine unakokujua Juha Wewe.
 
Back
Top Bottom