Hana tofauti na Jiwe maana kule Hazina, UVCCM,Makatibu Wakuu kote kaweka ndugu
Ukawa ya Malawi imechokwa kabla ya kuanza Kazi.β¦
This is Africa
Dogo taratibuNimeipata kutokea Gazeti hilo la The Citizen hivyo ningekuwa ni Mpumbavu kama Wewe niseme nimeitolea huko Kwingine unakokujua Juha Wewe.
"Lazaro" kafanya ma utopolo sana kuchagua mawaziri kiboya!!! Kosa alianza pale kwa waziri wa sheria yule aliyetosa uteuzi.Kuna Mtu Mmoja aliwahi kuniambia Mzukulu kuwa Waafrika wengi ni Watu wa Kupenda sana Mabadiliko na Ujio wa Vyama vingi katika Kushika Dola za nchi zetu hizi ila hapo hapo Waafrika tumesahau kwamba tabia zetu za Kiafrika zinafanana hata kama tutakuwa tunampenda na Kumuamini Mtu fulani kutokea upande tuupendao na kuuchukia ule atokao.
Ni kwamba katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ambayo pia imepelekea hata Wananchi wa Malawi ambao walimpigia Kura sasa Kujutia Kumuweka Madarakani Rais Mteule wa Malawi Mwinjilisti Lazarus Chakwera ameanza Mazingaombwe yake na Upuuzi wake kwa Kuteua Baraza la Mawaziri ambalo humo humo lina Ndugu na Mashemeji ikiashiria anatanguliza Undugu Serikalini.
Kwa kuanzia tu ameteua Waziri wa Kazi na wa Afya ambao wote Wawili ni Ndugu moja kwa Baba na Mama. Kuona hiyo haitoshi Kateua Waziri wake mpya wa Habari ambaye kumbe nae ni Shemeji wa Naibu Waziri wa Kilimo. Na kwa Kumalizia Upuuzi wake Rais huyu Kateua tena Waziri wa Usafirishaji ambaye tena ni Mume wa Naibu Waziri wa Ardhi.
Ndiyo maana kuna muda Mzukulu huwa nasema ni kheri tu nchi za Afrika ziendelee Kuongozwa na Marais Wakongwe kuliko Wapuuzi kama hawa.
Kwa anayetaka Taarifa hii Kamili ipo katika Gazeti la Mtandao la The Citizen.
"Lazaro" kafanya ma utopolo sana kuchagua mawaziri kiboya!!! Kosa alianza pale kwa waziri wa sheria yule aliyetosa uteuzi.
Mkuu mbona hata sisi hapa iko hivo fatilia hizi teuzi...pia hukumbuki ya magreth Sitta na Samuel SittaAfrica tuna nini lakini [emoji1787][emoji1787][emoji1787] dada yake, shemeji yake, mke wake [emoji119][emoji119]
Kuna jamaa humu anayejiita Erythrocyte aliandika eti Mungu mbariki Chakwera.Ukawa ya Malawi imechokwa kabla ya kuanza Kazi.β¦
This is Africa naamini mabeberu waendelee kutusimamia..Rais mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amekosolewa kwa kuteua Baraza la Mawaziri linalojumuisha Mtu na Mke wake pamoja na watu wengine ambao ni ndugu
Sidik Mia, ambaye ni Mgombea mwenza wa Rais huyo katika Uchaguzi wa mwaka 2019 amechaguliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi huku mke wake, Abida Mia akiwa Naibu Waziri wa Ardhi
Kenny Kandodo ni Waziri mpya wa Kazi huku dada yake, Khumbize Kandodo akiwa ni Waziri mpya wa Afya. Mfanyabiashara Gospel Kazako amekuwa Waziri wa Habari huku Shemeji yake, Agnes Nkusa Nkhoma akiwa Naibu Waziri wa Kilimo
Baadhi ya Wakosoaji wameshangazwa na Baraza hilo kwani Rais Chakwera amefanya kile ambacho aliwahi kumkosoa nacho aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kuhusu upendeleo na kuteua watu kutoka mkoani kwake
Wameongeza kuwa zaidi ya asilimia 79 ya Baraza jipya la Mawaziri wanatokea Mkoa wa Kati ambapo Rais Chakwera anawafuasi wengi
Sijui kama BAK kapita hapa. Nashikilia msimamo wangu kwenye ule uzi wa kutengua kinga ya kutoshitakiwa rais mstaafu ndani ya massa 24. Siamini watu wanaofanya maamuzi ya haraka bila sababu.
Rais mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amekosolewa kwa kuteua Baraza la Mawaziri linalojumuisha Mtu na Mke wake pamoja na watu wengine ambao ni ndugu
Sidik Mia, ambaye ni Mgombea mwenza wa Rais huyo katika Uchaguzi wa mwaka 2019 amechaguliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi huku mke wake, Abida Mia akiwa Naibu Waziri wa Ardhi
Kenny Kandodo ni Waziri mpya wa Kazi huku dada yake, Khumbize Kandodo akiwa ni Waziri mpya wa Afya. Mfanyabiashara Gospel Kazako amekuwa Waziri wa Habari huku Shemeji yake, Agnes Nkusa Nkhoma akiwa Naibu Waziri wa Kilimo
Baadhi ya Wakosoaji wameshangazwa na Baraza hilo kwani Rais Chakwera amefanya kile ambacho aliwahi kumkosoa nacho aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kuhusu upendeleo na kuteua watu kutoka mkoani kwake
Wameongeza kuwa zaidi ya asilimia 79 ya Baraza jipya la Mawaziri wanatokea Mkoa wa Kati ambapo Rais Chakwera anawafuasi wengi
Hii si iko saana hata ndan ya CDM...viti maalumu vimewalaza wengi sana.Ndugu anachokifanya au alichokifanya huyu Rais Chikwera ndiyo Picha halisi hata ya Wapinzani wengine tu tunaowataka Watawale nchi za Afrika.
Mbona trump kaweka watoto wake na wakweHii ndiyo Afrika......
Km mawaziri?!!! Kuweka kwenye ushauri si mbaya Sana...Mbona trump kaweka watoto wake na wakwe