Malawi Vs Tanzania Oktoba 11, 2015

Malawi Vs Tanzania Oktoba 11, 2015

Kivule

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
639
Reaction score
662
Baada ya mechi ya kwanza kuchezwa Dar es Salaam Oktoba 7 uwanja Taifa na Taifa stars kuibuka kidedea kwa mabao mawili bila majibu, leo ni hitimisho kwa mechi ya marudiano kutoka Malawi ambayo itaamua nani asonge mbele na nani iwe tamati kuelekea Urusi 2018. Taifa stars inahitaji ushindi wa aina yoyote, suluhu ama ushindi wa Malawi usiozidi goli moja. Stars kufunga goli lolote ugenini pia itazidi kuiweka Malawi kwenye hali ngumu kwani Malawi itahitaji kuanzia magoli manne kujinasua.

Tuwe pamoja kwenye mada hii kujuzana kile kinachojiri mechi ya The Flames Vs Taifa Stars kutoka uwanja wa Kamuzu. Taifa Stars imeshawasili mjini wa Blantire kwa basi kutoka Lilongwe ambako walitua. Kuingia uwanja wa Kamuzu inahitaji kuwa na angalau Kwacha 1000 sawa na Tshs 4000 kwa hela za nyumbani, mechi itarusha na Supersport 9 na wanaotumia king'amuzi cha Azam wanaweza kuona kupitia Malawi TV. kuanzia saa tisa kamili alasiri.

Kocha Mkwasa akiongea mapema kidogo amesema timu haina majeruhi na amesema kutakuwa na game plan tofauti kidogo na Nazir naye kasema leo watajitahidi kutoruhusu goli ili wajihakikishie kusonga mbele.

Kikosi cha stars leo kitakuwa na wachezaji wake mahiri.
  1. Ally Mustapha
  2. Shomari Kapombe
  3. Haji Mwinyi
  4. Kelvin Yondani
  5. Nadir Haroub
  6. Himid Mao
  7. Thomas Ulimwengu
  8. Mudathir Yahya
  9. Mbwana Samata
  10. Said Ndemla
  11. Farid Mussa
===========

00' Filimbi imeshapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo huu
35' Taifa stars wanakosa goli baada ya kufanikiwa kupata kona
42' Gooool, Malawi wanafunga bao la kwanza baada ya John Banda kutia nyavuni
1-0
44' Mudathir anapewa kadi ya njano na faulo inapigwa kelekea Malawi na Shomari Kapombe lakini haikuzaa matunda.
45+1' Mpira sasa ni mapumziko na matokeo yanasimama Malawi 1-0 Tanzania

46' Mpira umerejea baada ya mapumziko
60' Malawi wanafanya badiliko la wachezeji
70' Yondani anaondoa hatari langoni mwa Taifa Stars
72' Ulimwengu anawekwa chini na faulo kuelekea Malawi, Himid Mao anapiga lakini unatoka nje
73' Mustapha Bartez anaondoa mpira baada ya lango la taifa stars kuwa katika hatari
74' Mbwana Samatta anafika langoni mwa Malawi lakini mpira unatoka nje
76' Kuna sintofahamu na John Boko na Mzava wa Malawi wote wanapewa kadi za njano, mpira unaelekea Taifa stars
78' Mrisho Ngassa anaingia kuchukua nafasi ya Farid Mussa pia Malawi wanafanya mabadiliko
90' Malawi wanapata kona lakini haikuzaa matunda'
90' Zinaongezwa dakika nne
90+3' Samatta anapewa kadi ya njano baada ya kupanda na kushuka kwenye machela
90+4' Ulimwengu anabebwa kwenda nje
90+5' Pyeeee, kipenga kuashiria mwisho wa mchezo

Matokeo yanaisha kwa Stars kufungwa goli moja lakini wanasonga mbele baada ya kuongoza matokeo ya jumla kwa 2-1. Timu inarejea kesho na baada ya ushindi huu itakutana na Algeria.

 
Last edited by a moderator:
kikosi kiko poa. kila la heri Taifa Stars
 
AZAM wataonyesha au SUPERSPORT?.
Tupeane taarifa twendeni sawa!
 
Mungu Ibariki Taifa stars
Mungu lbariki Tanza nia
 
Eee Mwenyezi Mungu ibariki timu yetu na hakika irudi na ishindi wa kishindo. Bila shaka hii ni zamu ya Tanzania.
 
farid mussa namkubali ile mbaya huyu dogo kwanini asipelekwe arsenal kufanya majaribio AZAM watusaidie kwa hili
 
farid mussa namkubali ile mbaya huyu dogo kwanini asipelekwe arsenal kufanya majaribio AZAM watusaidie kwa hili

Kama nchi yako iko nje ya 70 bora za FIFA ranks, mchezaji marufuku EPL, unless mchezaji aende kama teenage, ajoin ktk soccer academy za club za EPL
 
Kama nchi yako iko nje ya 70 bora za FIFA ranks, mchezaji marufuku EPL, unless mchezaji aende kama teenage, ajoin ktk soccer academy za club za EPL

hii sheria imeanza mwaka gani mkuu tufahamishane. najua kufanya majaribio inawezekana na anasubir mda fulan apate kibal cha kazi au apelekwe nchi nyengne acheze kwa mkopo inatosha kwa farid nakumbuka kuna wachezaji kama ryo miaichi, campbell wote hawakuwa na kibal lakin walienda kwa mkopo timu nyengne na sasa wapo poa japo ryo aneachwa na arsenal kwasabab ya kiwango
 
hii sheria imeanza mwaka gani mkuu tufahamishane. najua kufanya majaribio inawezekana na anasubir mda fulan apate kibal cha kazi au apelekwe nchi nyengne acheze kwa mkopo inatosha kwa farid nakumbuka kuna wachezaji kama ryo miaichi, campbell wote hawakuwa na kibal lakin walienda kwa mkopo timu nyengne na sasa wapo poa japo ryo aneachwa na arsenal kwasabab ya kiwango

Sijui kuhusu Ryo, Ila kuhusu Campbell, utaifa wake (is it Costa Rica or Colombia) ulihusika! Wakati anasaini arsenal, alikuwa mfugaji bora wa world cup U21, na nchi yake ilikuwa juu at FIFA ranks
 
Back
Top Bottom