Malawi yatangaza siku tatu za maombolezo baada ya mawaziri wawili kufa kwa COVID-19

Malawi yatangaza siku tatu za maombolezo baada ya mawaziri wawili kufa kwa COVID-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri wa Serikali za Mitaa, Lingson Belekenyama na Waziri wa Usafirishaji, Sadik Mia wamefariki Januri 12 asubuhi kutokana na COVID19.

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera ametangaza siku tatu za maombolezo kwa ajili ya mawaziri na wamalawi waliofariki kwa COVID19.

Bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia Januari 12 hadi Januari 14.


1610477672614.png
 
Acha utani wewe, hii kitu ikikupata na kama afya yako siyo nzuri ni hatari sana. Yaani inakupa vichomi vya hapa na pale kwenye mapafu, uwezo wote wa kunusa unapotea.

Mwili unauma kama vile ulibeba kiroba cha kokoto, halafu kichwa kinaumwa na homa kama ya malaria vile.
Mkuu ulikuwa unapata tiba gani kwa kipindi hicho unachoumwa hadi kupona?
 
Kule Benosiurs kiongozi anaweza kufunguliwa mashtaka ya mauaji kwa kukataa kuwapa raia wake tiba.
 
Mkuu ulikuwa unapata tiba gani kwa kipindi hicho unachoumwa hadi kupona?
Homa yangu na kichwa kuuma ilikwa kwa masaa 12 ila uchovu wa hapa na pale na kupoteza uwezo wa kunusa ulikuwa kwa wiki mbili hivi.

Nilikuwa natumia tiba asili tuu, nilisaga kitunguu saumu (punje moja - vile vikubwa) na kuweka kwenye glasi ya maji na kunywa. Allicin, kemikali iliyo kwenye kitunguu saumu inazuia damu kuganda.

Virusi vya Corona huwa vinagandisha damu, wataalamu wanasema hii ndiyo sababu ya kuwa na vichomi kwenye mapafu na maumivu kwenye viungo. Pia Allicin huwa inafanya mishipa ya damu kutanuka (Vasodilation) hivyo kupunguza blood pressure.

Pia nilipiga sana nyungu, nilisaga mchanganyiko wa kitunguu saumu, malimao na tangawizi, nilichemsha na kujifunika kwa blanketi na kuhemea mvuke kutoka kwenye sufuria ya moto. Kitunguu pamoja na tangawizi vinaua virusi vya aina nyingi na hivyo ukihema mvuke wake unakwenda moja kwa moja kwenye mapafu na kuingia kwenye damu ndani ya sekunde chache sana.

Pia mara kwa mara nilisaga kitunguu saumu na kukinusa, allicin huwa ina "breakdown" mucus haraka sana na kuondoa pua kuziba. Vile vile hii allicin inafanya immune system kuwa "super alert".
 
Back
Top Bottom