Malaysia yaidhinisha Tsh. Bilioni 166.9 ili kuanza utafutaji wa Ndege ya MH370 iliyotoweka miaka 10 iliyopita

Malaysia yaidhinisha Tsh. Bilioni 166.9 ili kuanza utafutaji wa Ndege ya MH370 iliyotoweka miaka 10 iliyopita

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
1734694825398.png

Serikali ya Malaysia imekubali kuanzisha upya utafutaji wa Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH370, ambayo ilitoweka takriban miaka 10 iliyopita, ikiwa ni mojawapo ya matukio yaliyoshangaza sekta ya anga.

Siku ya Ijumaa, waziri wa uchukuzi wa Malaysia Anthony Loke alisema baraza la mawaziri liliidhinisha kimsingi mkataba wa $70m (£56m) na kampuni ya Marekani ya uchunguzi wa baharini ya Ocean Infinity kutafuta ndege hiyo.

Mpango huo uliopewa jina la "Bila Kuipata, Hakuna Malipo", kampuni ya Ocean Infinity italipwa fedha hizo endapo tu mabaki yatapatikana.

Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH370 ilitoweka Machi 2014 ilipokuwa ikielekea Beijing kutoka Kuala Lumpur ikiwa na Abiria 239.

Juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo aina ya Boeing 777 zimeenea kwa miaka mingi na mamia ya familia za waliokuwa ndani ya ndege hiyo zimesalia kuandamwa na mkasa huo.

Utafutaji wa awali wa mwaka 2018 wa Ocean Infinity chini ya masharti kama hayo uliisha bila mafanikio baada ya miezi mitatu.

Soma Zaidi: Mahakama ya China kuanza kusikiliza kesi dhidi ya Shirika la ndege la Malaysia kuhusu kupotea kwa ndege ya MH370

**********************

The Malaysian government has agreed in principle to restart the search for Malaysia Airlines Flight MH370, which disappeared nearly 10 years ago, in one of aviation's most enduring mysteries.

On Friday, Malaysia's transport minister Anthony Loke said the cabinet approved in principle a $70m (£56m) deal with US-based marine exploration firm Ocean Infinity to find the aircraft, News.Az reports, citing foreign media.

Under a "no find, no fee" arrangement, Ocean Infinity will get paid only when the wreckage is found.

Malaysia Airlines Flight MH370 disappeared in March 2014 while on its way to Beijing from Kuala Lumpur with 239 people on board.

Pia soma: Utafutaji mpya wa Ndege ya Malaysia Airlines MH370 waanza tena baada ya miaka 11

Efforts to locate the wreckage of the Boeing 777 have sputtered over the years and hundreds of families of those on board remain haunted by the tragedy.

A 2018 search by Ocean Infinity under similar terms ended unsuccessfully after three months.

A multinational effort that cost $150m ended in 2017 after two years of scouring vast waters.

While the government has "in principle" accepted Ocean Infinity's offer, Loke said negotiations over specific terms of the deal were still ongoing and would be finalised early next year.

The new search will cover a 15,000 sq km patch in the southern Indian Ocean.

"We hope this time will be positive," Loke said, adding that finding the wreckage would give closure to the families of those on board.

Flight MH370 took off from Kuala Lumpur in the early hours of 8 March 2014. It lost communication with air traffic control less than an hour after take-off and radar showed that it deviated from its planned flight path.

Investigators generally agree that the plane crashed somewhere in the southern Indian Ocean - though it is unclear as to why it happened.

Pieces of debris, believed to be from the plane, have washed up on shores of the Indian Ocean in the years after the disappearance.

A host of conspiracy theories have sprouted around the aircraft's disappearance, from speculation that the pilot had deliberately brought down the plane to claims that it had been shot down by foreign military.

A 2018 investigation into the aircraft's disappearance found that the plane's controls were likely deliberately manipulated to take it off course, but drew no conclusions about who had been behind it. Investigators said at the time that "the answer can only be conclusive if the wreckage is found".
 
Hela yote hii ya nini na watu walishadanja,
Anyway, huenda Kuna matumain ya kupatikana wakiwa hai 🏃🏃🏃
Nope Wale ni binadamu inahitajika evidence kama wamekufa ama walikumbwa na mkasa Gani. Some counties are very serious when it comes to the matter of life and destiny siyo huku kina Soka, Ben sa8 na wengine kibao wanapotea na mamlaka zinaona it is ok
 
Kuna nadharia ya kijasusi kuwa ndege ilitua Diego Garcia.
 
hawa jamaa utafiti wao wakauanzie pale diego garcia, watakuja kunishukuru wakichukua ushauri huu.
 
Kuna nadharia ya kijasusi kuwa ndege ilitua Diego Garcia.
ndege ilikaa angani masaa kadhaa zaid ya uwezo wa mafuta iliyokuwa nayo wakat inatake off, au ndege nayo huwa inagear ya free kusave wese?
 
Ni jambo zuri kufanya uchunguzi huu bila kujali zitatumika fedha kiasi gani. Naunga nkono hoja.

Hii itasaidia kufuta conspiracy theories nyingi tulizozisikia
 
No find no fee terms. Hiyo Co ya utafutaji itapata bonge la hasara.
 
Hii ndege haikupotea waanze uchunguzi kuhusu drone ya marekani iliyodondoshwa Afghanistan kisha ikagombaniwa na Russia na China mwisho China akafanikiwa kuidisassemble na kuipeleka Malaysia.

Mengine hakuna haja ya kuzungumza hapa, ila wale abiria wapo wanakula maisha US.
 
Hii ndege haikupotea waanze uchunguzi kuhusu drone ya marekani iliyodondoshwa Afghanistan kisha ikagombaniwa na Russia na China mwisho China akafanikiwa kuidisassemble na kuipeleka Malaysia.

Mengine hakuna haja ya kuzungumza hapa, ila wale abiria wapo wanakula maisha US.
Hizo ndiyo conspiracy theories zilizoenea. Nafikiri wakifannya uchunguzi independent watapata majibu
 
Hakuna habari iliwahi kuniumiza kama hiyo,ilinihuzunisha mno

Neno la mwisho la mwamba bwana Zaharie Ahmad Shah (pilot) lilikuwa GOOD NIGHT MH 370 hiyo ilikuwa March 8, 2014 ndege ikiwa na abiria 227 ambao hajawahi kupatikana hadi leo pamoja na juhudi zote za dunia kuitafuta
 
Wange mshirikisha na MWAMPOSA, maana anamawasiliano na Mungu, anaweza kupewa majibu ikawasaidia.
Na zile SATELITE haziwezi kuwasaidia, maana huko space wanapiga mi picha picha ya huko juu wanatuletea, au huwa nao wanatudanganya tu.

Mi nahisi ili potelea huko milima ya Himalaya, waendelee kusubiria theluji eyeyuke, ndege itapatikana na marehemu tutaona mabaki yao..
 
Hii ndege haikupotea waanze uchunguzi kuhusu drone ya marekani iliyodondoshwa Afghanistan kisha ikagombaniwa na Russia na China mwisho China akafanikiwa kuidisassemble na kuipeleka Malaysia.

Mengine hakuna haja ya kuzungumza hapa, ila wale abiria wapo wanakula maisha US.
Hivi ilikuwa drone au mtambo wa kuendesha unmanned fighter jets?!
 
Back
Top Bottom