Malaysia yaidhinisha Tsh. Bilioni 166.9 ili kuanza utafutaji wa Ndege ya MH370 iliyotoweka miaka 10 iliyopita

Malaysia yaidhinisha Tsh. Bilioni 166.9 ili kuanza utafutaji wa Ndege ya MH370 iliyotoweka miaka 10 iliyopita

Tofauti kati ya mtu mweusi na wengine, ndio hii hapa
Naam. Wakati jamaa wanahangaika kupata majibu ili siku za mbele matukio kama hayo waweze kukabiliana nayo, ngozi nyeusi inawaza waliokufa huku akisahau hawa walio hai wanaopanda ndege kila siku.
 
Hii story niliosikia pia wakati nacheza draft pale Mburahati.
kuna jamaa nilimsoma aliezea kwa upana sana jinsi ilivyotokea na jinsi China na vietnam walivyosaidia kuficha ukweli maana ndege ilianguka mile kadhaa toka fukwe ya Vietnam,

akaelezea matukio yaliyofuata kama coverup, behind the scene deals zilizopigwa ili kufichiana siri n.k,

NB/.
siku 2 hivi toka siku ya tukio kulikua na mazoezi ya kijeshi eneo lile yaliyowahusu US na washirika wake wa pande zile, hivyo lile eneo lilijaa aircraft carriers za kutosha plus radar za kutosha za kijeshi....... it was impossible ndege kubwa kama ile ipotee 'ghafla'
 
Serikali ya Malaysia imekubali kuanzisha upya utafutaji wa Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH370, ambayo ilitoweka takriban miaka 10 iliyopita, ikiwa ni mojawapo ya matukio yaliyoshangaza sekta ya anga.

Siku ya Ijumaa, waziri wa uchukuzi wa Malaysia Anthony Loke alisema baraza la mawaziri liliidhinisha kimsingi mkataba wa $70m (£56m) na kampuni ya Marekani ya uchunguzi wa baharini ya Ocean Infinity kutafuta ndege hiyo.

Mpango huo uliopewa jina la "Bila Kuipata, Hakuna Malipo", kampuni ya Ocean Infinity italipwa fedha hizo endapo tu mabaki yatapatikana.

Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH370 ilitoweka Machi 2014 ilipokuwa ikielekea Beijing kutoka Kuala Lumpur ikiwa na Abiria 239.
1740814080335.png
 
Back
Top Bottom