Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Wasalaam ndugu zangu,
Heri ya mwaka mpya 2018.
Binafsi nashukuru kudra za Mwenyezi Mungu kunifanya niuone huu mwaka mpya.

Dhumuni la kuanzisha uzi huu ni kutaka tufahamiane zaidi, tukosoane na turekebishane ili mwaka huu wa 2018 tulifanye jukwaa hili liende sawia kwa michango mbali mbali ambayo tutakiwa tunatoa.

Binafsi mimi naipenda sana JF,
Hili ni tanuli za fikra na natumaini mchango wetu ni mkubwa sana katika jamii ya Tanzania hata kama Serikali, vyombo vya habari na mashirika ya mbali mbali hawaukubali huu ukweli.

Humu ndani tunaishi kama ndugu,
Tunakosoana, tunasifiana, tunakashifiana na hata kutukanana lakini mwisho wa siku UKWELI UTABAKI kwamba KILA MWANA CHAMA ANAMHITAJI MWENZAKE, haijalishi ni tajiri, maskini, msomi au mtu ambaye hajasoma.

Binafsi naishukuru sana JF na wanachama wote. Mimi kama mwanachama nitaendelea kuipenda sana JF na ntazidi kuchangia kwasababu natumai kwa hichi kidogo nilicho nacho naweza kuwagusa watu wawili watatu ndani ya jamii yetu.......

NB1: Baada ya kusema haya yote naruhusu maswali na maoni mbalimbali kuhusu MALCOM LUMUMBA pamoja na maandishi yake humu ndani ya Jukwaa hasa hasa kule SIASANI, JAMII INTELLIGENCE na INTERNATIONAL FORUMS.....

Pia wale wenye madukuduku au kero naomba waseme hapa ili niwaombe msamaha na tuanze huu mwaka vizuri..........

NB2: Unaweza kuuliza swali lolote lile kuhusu MALCOM LUMUMBA lakini naomba lisilenge kumkashifu mtu yeyote yule.

Natanguliza shukrani zangu......
Young Malcom........

CC: Consigliere, cognition, hearly, MSEZA MKULU, mngony, ze kokuyo, espy, Dragoon, Baazigar, RRONDO, Victor wa happy, Red Giant, Da'Vinci , Tobinho, mtembea kwa miguu, born again pagan, God Heals, FisadiKuu, UncleBen, Quinine Mwitu, Complex
 
mkuu kwa maelezo yako naomba unieleze huu mwelekeo mpya wa North Korea!,je ni imegwaya baada ya US kupiga mikwala au ni danganya toto??
 
Binafsi Naitaji Maelezo Ya Kutosha Hapo Kuhusu Michango Ndugu Yangu
Tufanyeje ili tuweze kuwa na mijadala au mabandiko yenye uzito kwa jamii ya JF ??
(Hasa kule IF na JI, tutumie lugha ya malkia labda, au tuandike kwa lugha ya kiswahili au njia yoyote ile ili kuwafikia watanzania kwa kiasi kikubwa)
 
mkuu kwa maelezo yako naomba unieleze huu mwelekeo mpya wa North Korea!,je ni imegwaya baada ya US kupiga mikwala au ni danganya toto??
Mkuu hili siyo dhumuni la uzi huu,
Lakini kwasababu umeuliza ngoja nijitahidi kukujibu kwa kadiri ya uwezo wangu.

Mosi,
Korea Kaskazini anatamani sanaa kuungana na Korea Kusini. Ukweli ni kwamba mbali na yote haya wale wawili ni ndugu wa damu na hata mgawanyiko wao ulitokana na mataifa ya nje.

Ushahidi wa hili ni ile vita ya mwaka 1950-1953 ambayo Korea Kaskazini aliianzisha dhidi ya Korea Kusini ili aziunganishe nchi zote mbili kuwa moja. Kwasababu wakati wa Vita ya pili ya dunia Korea ilikuwa chini ya Japan na baada ya Japan Kushindwa basi The Grand Alliance (Marekani, Urusi na Uingereza) wakaigawa Kaskazini na Kusini na kuwela mpaka uitwao 38th Parallel.

Hivyo tangia siku ile Korea zote mbili japo ni maadui lakini bado wanatamani sana kuungana kama ndugu. Sema tatizo ni kwamba mataifa makubwa yananufaika na ule ugomvi.

NB: Kim kutaka mawasiliano na Korea Kaskazini siyo dalili ya woga bali ni dalili ya uungwana kwasababu maongezi ya namna hii hayajaanza leo hii. Isitoshe leo mchana Serikali ya Kim imesema haya maongezi hayawahusu mataifa makubwa kabisa na wasijaribu kusogea.

Pili,
Utawala wa Kim hauwezi kuogopa kipindi hiki kwasababu wanajua kabisa Marekani siyo mjinga kuwavamia. Vikwazo vya Umoja wa mataifa haviwadhuru kabisa na imeshashuhudiwa kwamba Warusi na Wachina wanamsaidia sana Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya kiuchumi.

Ili Marekani aweze kuvamia Korea Kaskazini kwa njia ya Kijeshi inabidi apeleke Muswada kwenye Baraza la Ulinzi na Usalama ili wapitishe azimio la Uvamizi wa Kijeshi kama walivyofanya kule mwaka Libya. Bahati mbaya sana Wachina na Warusi hawawezi kuruhusu hicho kitu kwasababu wanajua madhara yake.

Tatu,
Korea Kaskazini mbali na ujinga wote ule ina kiongozi mwenye upeo mkubwa na dunia pia ni Kijana. Ukweli ni kwamba anafahamu ili Korea iweze kutoka hapo ilipo itahitaji kufanya mabadiliko makubwa sana kimfumo. Hawawezi kutegemea Urusi na Uchina kila siku.

Vurugu zote hizi za Kim ni kutafuta kukaa mezani na mataifa makubwa ili yamhakikishie usalama wake kama ambavyo alifanyika miaka ya 1996 na baba yake. Lakini bahati mbaya Marekani hataki kukaa meza moja na Korea kwasababu itaonyesha udhaifu na itakuwa na madhara makubwa kwenye diplomasia yake.

Kim anajua kwamba ana muda mrefu sana kutawala, na ili afike mbali anahitaji kujenge uchumi wa nchi yake hivyo njia mbadala ni kutafuta mbinu za kujiepusha na kutengwa kwa nama yoyote ile. (Political Isolation)

NB: Aanchokifanya Kim ndicho anachokifanya yule bwana mdogo wa Saudi Arabia, kuna baadhi ya vitu analegeza ili nchi yake ifike mbali kiuchumi kwasababu huwezi kuwategemea Marekani na Mafuta tu kila siku. Ameahidi hadi kuruhusu wanawake kufanya baadhi ya mambo ambayo wanakatazwa.

Haya machache tu mkuu.....
 
Wewe ni kati ya wanaJF makini chifu bila shaka unasoma saana kama hausomi saana basi wewe ni mhadhiri kama sio

mhadhiri basi mwandishi wa habari kama zile za kina Jeff koinange[wa kipindi kile cha Niger lakini] bila kumsahau izzo.

Lengo sio kutaka kukujua nakupa hongera tu.
 
Wewe ni kati ya wanaJF makini chifu bila shaka unasoma saana kama hausomi saana basi wewe ni mhadhiri kama sio

mhadhiri basi mwandishi wa habari kama zile za kina Jeff koinange[wa kipindi kile cha Niger lakini] bila kumsahau izzo.

Lengo sio kutaka kukujua nakupa hongera tu.

Hahaha,
Shukrani sana mkuu wangu Daby.....
I appreciate this....
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Ka swali kadogo tu wala usinishangae.

Malcom Lumumba ni mtu wa aina gani? Elezea kwa ufupi.
Mkuu Mwifwa,
Mimi niko kama jinsi nilivyo humu ndani.
Napenda kujifunza, napenda kufanya sana mijadala mbali mbali na watu na pia mimi ni mtu ninayependa sana matani..(Imefika kipindi hadi wati wanashindwa kutofautisha The Joking Malcom na The Serious Malcom)

Zaidi zaidi,
Malcom Lumumba ni mchizi wa kitaa tu.
 
Mkuu Mwifwa,
Mimi niko kama jinsi nilivyo humu ndani.
Napenda kujifunza, napenda kufanya sana mijadala mbali mbali na watu na pia mimi ni mtu ninayependa sana matani..(Imefika kipindi hadi wati wanashindwa kutofautisha The Joking Malcom na The Serious Malcom)

Zaidi zaidi,
Malcom Lumumba ni mchizi wa kitaa tu.
Shukrani sana mkuu kwa jibu lako zuri
 
Mkuu Mwifwa,
Mimi niko kama jinsi nilivyo humu ndani.
Napenda kujifunza, napenda kufanya sana mijadala mbali mbali na watu na pia mimi ni mtu ninayependa sana matani..(Imefika kipindi hadi wati wanashindwa kutofautisha The Joking Malcom na The Serious Malcom)

Zaidi zaidi,
Malcom Lumumba ni mchizi wa kitaa tu.

Mjini siku hizi vijana wazee wote tunaongea lugha moja.

Usikute Malcom ni mzee mmoja wa makamo na mvi zake [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom