fuentte
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 2,809
- 8,032
Bwana Malcom Lumumba,napenda kukupa heshima stahiki kwa elimu unayoitoa hapa JF maana kimya kimya umekuwa ukiongeza wafuasi kadri siku zinavyoenda bila kujijua. Katika pitapita zangu leo tarehe 01.01.2019 nikakutana na huu uzi ulioandikwa 01.01.2018 nikaupenda na sijajutia usingizi wangu. Kwa kuwa uzi ulianzishwa kwa minajili ya kufunga na kufungua mwaka,naomba lengo liwe lile lile kila ifikapo mwisho wa mwaka kwa tarehe kama hii kuundeleza mjadala kwa ridhaa yako lakini.
Mchango wako Katika mjadala wa uhusika wa putin katika kuiinua rusia ya leo,umejaribu kugusia kuinuka huku ukilinganisha na maandiko ya manabii daniel,ezekiel,n.k. kama taifa ambalo limenuiwa kuwa hivi linavyokuwa,tafadhali naomba uniweke wazi zaidi huu unabii unahusiana vipi na rusia ya leo ya putin?
Kwa sasa vijana wengi wanapitia kipindi kigumu kulingana na mazingira ya kiuchumi taifa linamotupitisha kutokana na sera za mkulu wetu,kwa uzoefu wako katika mazingira kama haya ni ushauri gani unaweza kutoa kwa vijana ili kuendana na hali hii ? Maana kwa sasa nguvu na elimu ya chuo peke yake haionekani kufua dafu.
Asante sana kwa nyuzi zako mkuu