Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

Bwana Malcom Lumumba,napenda kukupa heshima stahiki kwa elimu unayoitoa hapa JF maana kimya kimya umekuwa ukiongeza wafuasi kadri siku zinavyoenda bila kujijua. Katika pitapita zangu leo tarehe 01.01.2019 nikakutana na huu uzi ulioandikwa 01.01.2018 nikaupenda na sijajutia usingizi wangu. Kwa kuwa uzi ulianzishwa kwa minajili ya kufunga na kufungua mwaka,naomba lengo liwe lile lile kila ifikapo mwisho wa mwaka kwa tarehe kama hii kuundeleza mjadala kwa ridhaa yako lakini.

Mchango wako Katika mjadala wa uhusika wa putin katika kuiinua rusia ya leo,umejaribu kugusia kuinuka huku ukilinganisha na maandiko ya manabii daniel,ezekiel,n.k. kama taifa ambalo limenuiwa kuwa hivi linavyokuwa,tafadhali naomba uniweke wazi zaidi huu unabii unahusiana vipi na rusia ya leo ya putin?

Kwa sasa vijana wengi wanapitia kipindi kigumu kulingana na mazingira ya kiuchumi taifa linamotupitisha kutokana na sera za mkulu wetu,kwa uzoefu wako katika mazingira kama haya ni ushauri gani unaweza kutoa kwa vijana ili kuendana na hali hii ? Maana kwa sasa nguvu na elimu ya chuo peke yake haionekani kufua dafu.

Asante sana kwa nyuzi zako mkuu
 
Swali langu ni hili,
Wewe Umejikita katika usomaji wa vitabu vya aina gani au unapendelea kusoma vitabu vipi vya siasa,siasa ya Ulimwengu,uchumi,falsafa,dini,Autobiography,Biography,sports,kung fu na vinginenvyo au chochote kilichombele yako halali yako....???

Nasitaki kuamini kama humpenzi wa kusoma vitabu.

Shukran/Ahsanteee.
Ndiyo nasoma vitabu, japo huwa sisomi kila kitabu kilicho mbele yangu kwasababu sipendi kuona ujinga ukikatisha kwenye ubongo wangu. Nasoma vitabu vinavyohusiana na taaluma yangu na mambo mengine yenye umuhimu ndani ya jamii ninayoishi. Naamini ntakuwa nimekujibu vizuri mkuu.
 
Ndiyo nasoma vikitabu kipi ulichokisoma kikakupendezabu, japo huwa sisomi kila kitabu kilicho mbele yangu kwasababu sipendi kuona ujinga ukikatisha kwenye ubongo wangu. Nasoma vitabu vinavyohusiana na taaluma yangu na mambo mengine yenye umuhimu ndani ya jamii ninayoishi. Naamini ntakuwa nimekujibu vizuri mkuu.
Heri ya mwaka mpya mkuu long time no see you.
Swali. Je mwaka 2018 ni kitabu kipi ulikisoma kikakuvutia zaidi.. mention them
 
Kwa sasa vijana wengi wanapitia kipindi kigumu kulingana na mazingira ya kiuchumi taifa linamotupitisha kutokana na sera za mkulu wetu,kwa uzoefu wako katika mazingira kama haya ni ushauri gani unaweza kutoa kwa vijana ili kuendana na hali hii ? Maana kwa sasa nguvu na elimu ya chuo peke yake haionekani kufua dafu.

Asante sana kwa nyuzi zako mkuu
Nashukuru sana mkuu. Ushauri wangu ambao kwa watanzania wote kwa ujumla ni kwamba pale ambapo huwezi kuzalisha kwa kiwango ambacho kinaweza kukidhi mahitaji yako njia rahisi ya kuweza kuishi ni kubana matumizi tu. Tujitahidi kupunguza matumizi yasiyo na tija na kuwa na nidhamu na pesa. Huwezi kuwa na akaunti ambayo hiyohiyo ni ya mshahara, hiyohiyo matumizi na hiyohiyo akiba. Fungua akaunti nyingine anza kuwuke akiba huko, kama pesa hutaitumia leo basi utaitumia kesho, na kama huna mkakati maalumu kwa wakati huo ni heri hiyo pesa uiache tu huko benki kuna siku utakuja kupata wazo jema na utaitumia kulifanikisha hilo wazo lako. Lakini kama hakuna umuhimu wa kutumia pesa leo basi iache tu na utatumia hata kesho.
 
Heri ya mwaka mpya mkuu long time no see you.
Swali. Je mwaka 2018 ni kitabu kipi ulikisoma kikakuvutia zaidi.. mention them
Biblia huwa inanivutia kila mwaka nadhani kuliko kitabu chochote kile. Japo mwaka 2018 pia nilivutiwa sana na kitabu cha Easternization : War and Peace in the Asian Century.
 
Biblhuwa inanivutia kila mwaka nadhani kuliko kitabu chochote kile. Japo mwaka 2018 pia nilivutiwa sana na kitabu cha Easternization : War and Peace in the Asian Century.
Ipo hivo, unavyosoma biblia roho wa Mungu akikushukia ndio unazidi kuona biblia ni mpya na utagundua/unafunuliwa hekima ambazo hukuwa umeziona kabla.
Ahsante.
Labda taja vingine mkuu...
Swali. Kwanini hua unajikita sana kusoma vitabu vya namna hiyo
 
Mjini siku hizi vijana wazee wote tunaongea lugha moja.

Usikute Malcom ni mzee mmoja wa makamo na mvi zake [emoji23] [emoji23]
Kumbe ulidhani mtoto mwenzio!!![emoji85][emoji85][emoji85]
Ni libabu kweli kweli.
 
Swali. Kwanini hua unajikita sana kusoma vitabu vya namna hiyo
Mapenzi, lakini pia huwa napenda kufahamu kinagaubaga mambo yanoyeendelea duniani pamoja na athari zake kwangu.
Labda taja vingine mkuu...
The Prize: The Epic quest for Oil, Money and Power, Praetorian: The Rise and Fall of Rome's Imperial Body Guard, Death by China.
Hivi navyo vilinivutia sana.
 
Ahsante mkuu.
Je naweza kuvipata??
 
Kumbe ulidhani mtoto mwenzio!!![emoji85][emoji85][emoji85]
Ni libabu kweli kweli.
Sorry mkuu kwa kuingilia.
Mtoto una m-define vipi???
I mean mtoto ni nani??
Nasubiri jibu kako
 
Ndiyo nasoma vitabu, japo huwa sisomi kila kitabu kilicho mbele yangu kwasababu sipendi kuona ujinga ukikatisha kwenye ubongo wangu. Nasoma vitabu vinavyohusiana na taaluma yangu na mambo mengine yenye umuhimu ndani ya jamii ninayoishi. Naamini ntakuwa nimekujibu vizuri mkuu.
Nimependa sana hii comment Mkuu Malcom hasa hapo kwenye kulisha ubongo ujinga. Barikiwa zaidi, Heri ya Mwaka Mpya kaka
 
Mkuu Lumumba kwa Tanzania miaka ya nyuma tulikuwa tumeachwa mbali sana na Kenya kiuchumi miaka ya hivi karibuni tumepiga hatua kubwa kiuchumi karibia tunalingana.Tanzania ifanye nini iweze kuongoza kiuchumi Afrika mashariki?
 
Back
Top Bottom