Huyu ni yule daktari wa binadamu aliyeutosa udaktari na kuchangamkia ulanguzi wa pamba. Niliwahi kuhoji digrii zake hapa maana niliona kama zina utata, lakini baada ya uchunguzi nikagundua ni kweli alihitimu udaktari pale Muhimbili. Zaidi ya hiyo digrii ya udaktari, ana digrii nyingine mbili za magirini ambazo kazipatia oline kwenye vile vyuo feki maarufu kama 'degree mills'. Katika uchunguzi wangu niligundua mengine mawili:Mazee kama wabunge wenyewe ndio type hizi tunazoziona hapa (CHADEMA Regia Mtema, CCM Hamis Kigwangala ) basi tumekwisha.
Hamna CHADEMA wala CCM, kwa mtaji huu wote waganga njaa tu.
Kwanza, ndiye aliyekuwa kiongozi wa ule mgomo maarufu wa madaktari Muhimbili ambapo walialika bendi ya matarumbeta kuwaburudisha wagomaji wakati wagonjwa wakiendelea kufa kwa kukosa tiba. Baada ya hapo, baraza la madaktari lilimwekea sanctions kwa kitendo hicho cha kukiuka maadili ya kitaaluma, amefutiwa usajili kwa hiyo haruhusiwi kufanya kazi ya tiba popote duniani, na ndiyo maana amejikita kwenye biashara ya pamba.
La pili nililogundua ni kwamba huyu ni mmojawapo wa vibaraka wa Rostam Aziz, na pesa yote aliyotumia kwenye kampeni ni ya Rostam kwa lengo la kumuadhibu Lucas Selelii. Ndiyo maana Selelii hajateuliwa licha ya kushika nafasi ya pili, wakamchukua huyu wa nafasi ya tatu!