Malecela ahofia CCM kuwa katika hali ngumu 2010
*ASEMA WABUNGE WENGI WATABWAGWA
Jackson Odoyo na Neema Rugemalira
MAKAMU Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, John Samuel Malecela amekitabiria chama hicho wakati mgumu katika uchaguzi mkuu ujao 2010.
Akijibu swali la waandishi kuhusu ufisadi na uchaguzi ujao wakati akikabidhi vifaa kwa walemavu vilivyotolewa na Askofu wa Kanisa la Christian Mission Fellowship, Mgullu Kilimba jana, Malecela alisema chama hicho kitakuwa na wakati mgumu kutokana baadhi ya wabunge wake kutotekeleza ilani ya chama na vita dhidi ya mafisadi.
Uchaguzi mkuu ujao utakuwa mgumu kwa CCM hasa wabunge kwa sababu baadhi yao hawaendi majimboni na hawafuati ilani ya CCM. Ugumu mwingine upo katika suala zima la mafisadi, alisema Malecela na kuongeza:
Vita dhidi ya mafisadi ni ngumu kwa sababu ndani ya CCM kuna baadhi ya watu wanaokichafua chama kwa tabia zao za kuungana na mafisadi.
Mzee Malecela alisema hayo wakati tayari kukiwa na mvutano mkubwa ndani ya CCM baina ya kambi zilizojengeka ndani ya chama, huku kila kambi ikiituhumu nyingine kwa ufisadi.
Malecela alisema baadhi ya wabunge wa CCM wanakiweka chama hicho katika wakati mgumu kwa sababu ya tabia zao za kutokwenda kwenye majimbo yao na kwamba, hawafuati ilani ya uchaguzi ya chama hicho.
Hata hivyo, akizungumzia uchaguzi wa rais alisema atakuwa na wakati mzuri kwani kwa upande wake hali bado ni njema.
Alisema pamoja na jitihada za mafisadi kutafuta kila njia ya kuungwa mkono na baadhi ya wana CCM ndani na nje ya bunge, ukweli ni kwamba vita hivyo ni vigumu na kwamba anaamini kuwa mwisho wa siku wapinga ufisadi watashinda.
Tunaopiga vita suala la ufisadi ndani ya CCM tutaendelea kusimama imara mpaka dakika za mwisho, mfano mzuri ni kile kilichotokea kwenye mkutano wa Bunge safari hii, nadhani mliona mambo yalivyokuwa moto. Hii yote ni kuhakikisha kuwa mafisadi yanashindwa, alifafanua Mzee Malecela.
Akitaja baadhi ya mambo ambayo mafisadi hayo yalipanga yafanyike ndani ya bunge hilo lakini wakashindwa, Makamu Mwenyekiti huyo mstaafu alisema kuwa ni pamoja na suala la uchimbaji wa madini kwenye mbuga za wanyama, Richmond pamoja na mgodi wa Kiwira.
Ndugu zangu ninawaambia, Tanzania ya leo hakuna uwezekano wa mpiga kura kununuliwa, watajaribu watashindwa; sana sana watajaribu kuleta hizo fedha zao ziliwe na wasipate kura na hiyo ndiyo njia pekee ya Mungu kuwaadhibu, kwa sababu hizo ni fedha za wananchi, aliongeza Malecela.
Hata hivyo alisema watakapo fanikiwa kuzima moto wa mafisadi kazi yao itakuwa ni moja tu ya kupambana na wapinzani wao ambao nao watajitahidi kutafuta mbinu za kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo.
Baada ya vita vya mafisadi kumalizika tutabakia kazi ya kupambana na wapinzani wetu kwa sababu wao pia wanatafuta mbinu za kushinda uchaguzi ingawa tuna mbinu nyingi za kuwashinda, alifahamisha Malecela.
Alisema CCM ina mbinu nyingi na hawajawahi kuzitumia zote katika chaguzi zao na kwamba, baadhi ya mbinu mpya walizonazo walizitumia katika chaguzi ndogo zilizopita hivi karibuni na wakaibuka kidedea.
Tuna mbinu nyingi za kuwashinda wapinzani wetu, baadhi yake zilitumika katika chaguzi zilizopita na katika uchaguzi mkuu mwaka ujao tutazindua mbinu mpya ambazo hatujawahi kuzitumia.
Katika hatua nyingine Malecela alisema kutokana na vita hivyo kuwa vikali, ndiyo maana Spika wa Bunge, Samuel Sitta alisema kuwa matatizo makuu yanayowakabili ni vita dhidi ya mafisadi.
Vita ni vikali na mimi sina shaka yoyote kwamba mafisadi hao watashindwa, isipokuwa tunapaswa kuendeleza kasi ya kupambana nao.
Malecela alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh58 milioni kwa walemavu vikiwemo viti, baiskeli za magurudumu matatu, vyoo magongo ya kutembelea na vingine vilivyotolewa na Kanisa la Christian Mission Fellowship.
Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwa mzee Malecela jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela.
Askofu Kilimba wa kanisa hilo amesema tangu waanze kutoa huduma hiyo miaka minne iliyopita, wameishayafikia majimbo ya uchaguzi 38.
***************************************************
Afadhali amekubali kwamba mwakani ngoma itakuwa nzito sana, na kitakachowatesa ni hizo agenda za ufisadi.
Je, yaliyotokea juzi Bungeni inaweza kuwa ni sanaa ya CCM kuwahadaa wadanganyika kwamba wabunge wao (majority wakiwa wa CCM) wako makini kutetea maslahi ya taifa?
Hizo mbinu walizonazo ni zipi? Wizi wa kura ama kutumia jeshi la polisi na tume ya uchaguzi ama ni zipi hizo?
Kwanini kwenye ufisadi haongelei KAGODA? Maana wameikalia kimya kabisa as if imesahaulika.
Ngoja tuone sanaa ya Bunge kwenye kikao cha 18 mwezi Novemba.