Elections 2010 Malecela ahofia CCM kuwa katika hali ngumu 2010

huyu mzee bwana!............amesahau kwamba alishataka kuwa USTAADHI kwa tamaa za pesa!
 
 

- Sasa nielemishe jinsi kiongozi anayefaa kama Kambarage kuishia kuchagua viongozi wasiofaa, huku akijua hawafai ili walifanyie nini taifa? Kwa hiyo unasema Mwalimu alikuwa akichagua viongozi wasiofaa makusudi just because ana sababu! labda uiseme ni sababu ipi hiyo?

- Eti hizi ni logic au facts? Huwezi kunikwaza bila ya kuwa na facts ya unachokisema, infact unajikwaza mwenyewe so far, au?

Respect.

FMEs!
 

- Hii ninamuachia Mkulu Engineer aje kujibu, maana mimi siwezi mapigo haya BWa! ha! ha! ha! ha!

Respect and Out!

FMEs!
 


Mkuu FMES watu hubadilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine. Mzee alivyokuwa yaani zile colours alizokuwa nazo at that time Nyerere anamchagua kuwa kiongozi huko kote ulikosema si hizi alizokuwa nazo baada ya Mwalimu.
Huyu huyu alikuwa wa kwanza pamoja na kundi lake kulizika azimio la Arusha.
Na ni kwa huyu huyu Nyerere alijuta kumuweka kwenye system yake hadi kamtungia kitabu. Ina maana kama Nyerere angepewa nafasi ya kutawala tena nakwambia hata anayozungumza leo asingeweza kusema neno.
Na unaweza kuona kweli kwamba huyu sasa anaonyesha true colours kwa uoza anaosema leo bila hata haya.
Hivi wizi wa kura na mbinu zingine chafu ni vitu vya kujivunia kwa mtu kama mzee huyu? Au labda tuseme uzee unamfanya mtu apunguze uwezo wa kufikiri kabla ya kusema?
Respect mkuu
 
- Kwa nini hakuiba kura za Tarime? Au Kigoma kwa Zitto? Acha kurukia treni mkuu na habari za kusimuliwa na alinacha, tafuta facts mwenyewe kabla ya kukurupuka na lugha za hovyo hovyo ambazo haziwezi kutusaidia taifa mkuu Bwa! ha! ha! tizama unavyojikanyaga kanyaga Ha! ha! ha! Inawezekana haya ya uzee una experience nayo, labda ungetoa definiton kwanza on uzee, maana kama wewe kijana unashindana na Mzee Malecela kila kukicha anakushinda kwenye uchaguzi, then something is wrong na hii theory yako ya uzee, kwani Makamba sio mzee mbona hakushinda Tarime? Kwa nini wazee Makamba na Msekwa hawakuiba kura Tarime?

- Anyways samahani nilitaka tu kukupa darasa kidogo tu juu ya tabia ya kudandia treni kwa mbele, sasa unaweza kuendelea na matusi yako, Bwa! ha! ha! Ndugu a great thinker ndani ya The home of the great Thinkers!

Respect.

FMES!
 
Mzee pamoja kwamba huyu mzee ni baba yako , lakini kwa maneni yake haya nadhani anastahili kulaaniwa .Bura nzuri ni kama nyie mtamshauri akae pembeni sasa amesha choka na wenzake kama akina Kingunge wana haribu.Yes Tarime hawakuweza kwa kuwa wanaume walisimama kule .Kote kote alikosimamia aliendesha zoezi wa wizi wa kura si kuiba ma box bali kupora ushindi kwa kusema sisi ni Serikali Tangaza tumeshinda na ikawa hivyo .
 

MvutaKamba unanipa raha!
 

- Labda ni baba yako wewe, ila hapa JF huwa hatujali baba wa nani tunakata ishu tu bila uoga wala vitisho au kuogopa matusi, kwenye siasa kuna laana ya wananchi na huionyesha kwenye vibox vya kura.

- Lakini hao wanaume wakashindwa kusimama Biharamulo na Busanda, another mufilisi theories, kwa hiyo una maana katika majimbo yote ya Tanzania, ni Tarime peke yake kwenye wanaume huku kwingine ni wanawake watupu? Bwa! ha! ha! pole sana great thinker!

- Na how do you define wanawake wa majimbo mengine ya Tanzania na hii theory yako ya siasa za wanaume na wanawake?

- Sasa kaanze kuwaondoa wazee kina Ndesamburo na Slaaa, halafu uhamie CCM, huyu baba yako aliweza kuiba kura kwingine kote lakini akashindwa kuiba Taarime na Kigoma, si unaona unavyochekesha! Bwa! ha! ha!

- Mapovu mengi kama una hoja kumbe ni mtupu kama aliyekutangulia! ya kudandia treni kwa mbele unaona sasa aibu na huyo baba yako! Bwa! ha! mkuu naona ndio kwanza umeingia hii JF hapa huwa hatujali baba wa mtu wala wa member huwa ni fimbo tu! Hoja hujibiwa kwa hoja na viroja hujibiwa na viroja,

- karibu sana JF, maana ninakukumbuka kutoka forums moja kule vichochoroni, hapa umeingia kwenye ngoma kubwa, yaani the home of great thinkers sasa jaribu ku-adjust maana hapa ya baba hayana nafasi ni taifa mbele tu na masilahi yake!

Respect.

FMEs!
 
Wee mvutakamba,
Walishatuonya kuhusu kumsema mzee wetu kwa nini umethubutu?
Sasa unaona mashambulizi?
Masanilo asante kwa kutupa tahadhali. Hata hivyo message sent.
 
Kwa hakika ni mwelekeo mzuri, lakini inafaa wengi wapate ujasiri na kuanza kuzungumza na wazungumze kwenye vile vikao rasmi, ni wakati wa kuachana na zidumu fikra...

Unajua ndani ya Chama Makamba amehakikisha kuwa agenda ya ufisadi haijadiliwi katika vikao halali vya chama na hili kwa kiasi fulani amefanikiwa.Kwa kuwa hilo limetokea wanachama wa CCM hawana fursa nyingine ya kusema ufisadi wazi wazi isipokuwa kwenye vyombo vya habari,na kwenye mikutano yao isiyo rasmi.

Mimi naona huu ni mwanzo tu wa mambo mazuri kuja hapo baadae ambapo wanachama wa ccm wataacha uoga na kuelezana ukweli wazi wazi.Unajua kuna wazee waliobobea kwenye siasa kama Mzee Malecela ukitaka kumtuhumu katika vikao halali ndani ya chama lazima uwe umejipanga kweli kweli na umejiandaa vya kutosha kwa hoja yako.Vinginevyo hoja yako itakurudia wewe mwenyewe na kuishia kuadhibiwa na chama.

Mimi nachukia ufisadi na wizi wowote wa rasilimali za Tanzania,wizi huu ni pamoja na wizi wa kura kwani kwa kufanya hivyo kunawanyima watanzania walio wengi fursa ya kupata viongozi watakao waletea maendeleo.Kwa hili Mzee Malecela hana pa kuponea ni lazima awaombe watanzania msamaha kwa kuwachagulia viongozi/wabunge kwenye chaguzi ndogo ndogo ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha kupwaya katika masuala ya uongozi.

Dawa ya ufisadi Tanzania tufanye kama China,kiongozi akituhumiwa kwa ufisadi anaachia madaraka kupisha tume huru kufanya uchunguzi.Na ikigundulika kuwa ameshiriki kwenye ufisadi au ubadhirifu wa mali ya umma ananyongwa hadharani na mali zake kutaifishwa na kuwa mali za serikali.

Tutakapo pata kiongozi mkuu wa nchi anayeweza kusimamia hili Tanzania tutaruka kwenda mbele katika maendeleo.Mfano wa nchi ya China kuwaadhibu mafisadi ni mfano wa kuigwa na kila kiongozi mwanamapinduzi apendaye maendeleo ya watu wake.Kinyume cha hapo ni usanii tuu ambao hauna maana katika uongozi.
 
Ufisadi kwa makada wa CCM ni siri na budi uongelewe ndani ya vikao vya Chama na si barabarani. Mjumbe CCM amewajia juu wanaotabiri CCM kupata wakati mgumu kwenye uchaguzi ujao na kuanika siri za chama kwa kuwahusisha baadhi ya viongozi na ufisadi !

Asante mjumbe - kumbe ufisadi ni sera ya siri ya CCM, kaazi kweli kweli, duh !
 
Hakika sasa wanaanza kuumbuana hadharani sisi yetu macho.
 
Naye mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Bw. Salum Londa amesema viongozi na wanachama wa CCM wanaokitabiria mabaya chama hicho wanatia shaka.


Huyu ndiye Salum Londa, Meya na kinara wa mipango ya ufisadi wilayani Kinondoni - akiwataka wanachama wa CCM kutokuwa tayari kupokea kauli za viongozi au wanachama ndani ya chama hicho eti wanaopiga vita ufisadi.


Huyo ndiye mtuhumiwa wa ufisadi wa viwanja Kinondoni anayetaka wale wote wanaodai kupiga vita ufisadi ndani ya CCM watoswe ili boti isizame.. wabaki mafisadi tuuu !
 
Naye KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amepinga kauli ya makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela kwamba, chama hicho kitakuwa na wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu ujao.


Huyu ndiye Yusufu Makamba, aliyedai EPA ni mambo ya kufikirika tu na kuyaita uzushi. Makamba anayedai CCM yake haikufaidika kwa namna yoyote na KAGODA. Masikini Makamba yuko tayari kufa na tai shingoni !!
 
Hivi ni nani asiyejua kuwa Londa ni fisadi na mchumia tumbo. Kuchaguliwa kuwa mjumbe wa NEC kwa kumshinda Shy-Rose Bhanji kwa kariibu anataka kuonesha kuwa na yeye mrija wake umeongezeka kipenyo na umeshaingia kwenye buyu kubwa la asali. Ukweli ni kwamba TINGA TINGA alichoongea amekifanyia utafiti from the ground (field work) si yeye ndiye alikuwa "BUSANDA" na "BIHARAMURO" ambako anajua fika kuwa hawakushinda bali waliiba kura!. Sasa kazi itakuwa ngumu mwakani kuiba kura majimbo yote!?, Hawa vibaraka waache woga, maisha hayapo kwenye 10% tu za miradi, wafanye kazi kama wanataka kuendelea kupata " KURA" siyo longolongo kwani zina mwisho wake.
 
Naye NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga amesema makada wa CCM wanaodai kupambana na ufisadi wanapaswa kudhibitiwa ili wasikivuruge chama kwa kuwa mafisadi ndani ya chama hicho hawazidi wanne.


Kaazi kweli kweli !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…