Calnde
JF-Expert Member
- Oct 7, 2008
- 1,373
- 278
Ni John Malecela, mumewe Anne Kilango,
Ameona matatizo ya mgomo wa vyuo vikuu, akatafakari kwa makini, akaona kwake yeye suluhisho ni kuwafukuza wote walioogoma na kuwapa udahili wale ambao waliomba nafasi wakakosa. Kwamba hakuna haja ya serikali kuhangaika na watu wasiojua umuhimu na maana ya elimu!
Amenipa nafasi nitafakari,
Je,kama serikali ikifanya hivyo,na hao watakaodahiliwa mara ya pili wakagoma watachukuliwa akina nani?
Na je, katika sakata la walimu na makundi mengine wanaogoma kudai haki zao kwa mtazamo wake nini kifanyike?
Hapo akanipa zaidi nafasi ya kujiuliza, Kama angeupata uraisi mwaka 2005 kama alivyokuwa akitamani, hali ingekuwaje? Angetatua vipi matatizo ya wananchi?