Wakuu zangu,
Kwanza samahani sana kuingilia mjadala ambao upo katikati.. Hivi mnapojiuliza Kama Malecela angekuwa rais ingekuwaje! mnajaribu kusema kitu gani maanake nashindwa kabisa kuliweka swala hili akilini. Kwangu binafsi ni sawa na mwanamke anayejiuliza kama ningeolewa na fulani ingekuwaje!.. sijui hizo hisia zinatoka kitandani, hali na mali ya maisha ama kitu gani..
Huyu Malecela mnamtazama kwa kitu gani hasa - Kwa kutazama maendeleo ya mtu huyo, biography ya mtu huyo, mafanikio ya mtu huyo au mapungufu ya mtu huyo..
Hapa nikiwa namaana maisha ya Uongozi hayawezi kupimwa kwa dhana..unless unacho kipimo cha Tanzania iko vipi, na ingekuwa vipi kulingana na mtu huyo..navyoelewa mimi hadi sasa hivi Tanzania inapimwa kutokana na viongozi waliopo/tangulia. Hakuna kati yetu alioyejua Tanzania ingekuwa vipi wakati Mwinyi akiingia madarakani! Mkapa au Kikwete isipokuwa tumekuja gundua kuwa wote ni BOMU na sijui niseme Tanzania imekuwaje kwa kila mmoja wao...
This country is goin' down the drain na sijui ktk hilo drainage tutaweza vipi kupima mazuri wakati ni harufu tupu na mwisho wa drainage unajulikana..
Labda mnambie mnachokusudia ni kumrudisha hapa FMES ambaye kwa hakika hivi sasa kijiwe kimeota majani, hakuna habari mpya... Yaani tumefikia hata kujadili mzee Malecela na Salim hawa babu zenu - Watu ambao ni generation ya Nyerere! Haya Jokakuu anataka kumvua mzee wa watu hadharani wakati aliyoyafanya yamefanywa na wazee wetu Pamoja na viongozi wote Tanzania..
Ama kweli vijana mnakosa adabu..