Elections 2010 Malecela ang'oa mashine ya maji aliyokifadhili kijiji cha Mtera?

malecela anadaiwa kung'oa mashine aliyokifadhili kijiji cha mtera

Haki ya nani..uzee mwingine balaa tupu!! Au ana mpango wa kuihamishia jimbo la Same kwa mkewe?
 
Jamani si ya kwake alitoa ili wampe KULA sasa wamemnyima KURA unategemea nini? TINGATINGA kachukue na zingine zilizobakia,

CCM OYEEE!!!!!!!!!!!! Chukua Chako Mapema!!
 
sawa alivyo fanya mzee, ingawa ni rafiki yangu, cyntika yuko wapi? sasa mwele na sechelela watachota maji wapi? au wao watakuja na buylldozer zao? bila kumsahau jaji?
 
Shida kuamini....Wapi ushahidi?Coz hii itakuwa kali ya mwaka kwa mawanasiasa mweye calibre yake kufanya hayo itakuwa too low....Inakuwa vigumu kuamini kuwa eti alikwenda kuing'oa mashine yamaji...Maji ni uhai wakuu.
 
Tingatinga limeniacha hoi, alitoa msaada au aliwaazima tu wanakiji?<p> </p>
<p>&nbsp;</p>
 
Sioni tatizo hapa kama mashine ile ni mali yake na alikuwa anawaazima wapiga kura waka kama mbunge wao. Sasa ana haki ya kuchukua mali yake hiyo kwa vile siyo mbunge wao tena. Mwaka 1965 ujerumani ya magharibi walibomoa barabara walizokuwa wanatujengea hapa Dar na kuiacha Nkurumah Hall bila kuimaliza wakati tulipokataa kuvunja uhusiano na ujerumani ya mashariki wakati huo itakuwaje Mzee Malecela asifaye yaliyo ya muhimu kwake.

Ukitaka kula lazima uliwe, watu hao wamekataa kuliwa basi hakuna kula tena
 
Kingunge mchonganishi yanamhusu nini ya mtera kwani alikuwepo wakati wanapeana?.Afunge bakuri lake huyo mzee nasikia anajiandaa kuwabwatukia maaskofu kwa mara nyingine.

"Kingunge" siyo jina la Mtu kama umjuavyo wewe na mimi, ni cheo/wadhifa ( Status)
 
Ni vyema wakaelewa ya kuwa kwa CCM misaada ni mikopo yenye masharti mazito na wala siyo vinginevyo.
 
iwe kweli au la... kwa mtu aliyewahi kuwa balozi, waziri mkuu nk... ni aibu jimbo lake lilivyochoka; watu wamechoka na mifugo imechoka...

alitakiwa awe out zamani sana....
 
Taarifa utoe wewe halafu wengine wakujuze!Duh,kweli hapa ipo kazi!
 
Kingunge mchonganishi yanamhusu nini ya mtera kwani alikuwepo wakati wanapeana?.Afunge bakuri lake huyo mzee nasikia anajiandaa kuwabwatukia maaskofu kwa mara nyingine.

No no sidhani kama aliyeandika alikuwa na maana Kingunge Ngombale Mwiru, mimi nimemuelewa tofauti kuwa alikuwa na maana Kingunge ni mtu mzito ndani ya ccm au kwa maneno mengine Kigogo. Mtake radhi mzee Kingunge Mwiru
 
Ndugu Kichuguu i cant believe this is coming from you.Yani viongozi waalendo wa act kama wakoloni dhidi ya wananchi?Mfano wako ni extremelly irrelevant.Uhusiano kati ya makaburu na wananchi kamwe siyo jambo jema kuufananisha na uhusiano wa viongozi wazalendo na wananchi..And if thats the case then change is imminent.
 
niliposema mkuu mwenye taarifa zaidi atujuze nilimaanisha kama, mfano, kuna picha ya hiyo mashine iliyong'olewa; lakini taarifa ni ya uhakika 100% kwani siyo siri tena kwa mkazi yeyote wa hapa idodomya.
 

Ndugu yangu JM, hawa viongozi wetu wa karibu nchi zote za Afrika, wamekuwa kama wakoloni machoni pa wananchi wao. Sababu ni kwamba kwa kipindi chote walicho tawala baada ya wakoloni kuondoka wamekuwa wakiwakandamiza, wamewanyonya na kuwapuuza wananchi wao kana kwamba wamekuwa vibaraka wa wakoloni. Ndiyo maana, nchi kama Nigeria, kenya, Jamhuri ya afrika ya kati, mali, togo viongozi wanaonwa ni sawa tu na wakoloni, ila tofauti ni kwamba wakoloni hawa ni weusi kama wananchi wenyewe.
Hata nyumbani TZ, wananchi tuliowengi tunashindwa kuwatofautisha viongozi wetu na wakoloni. Tunashindwa kuitofautisha CCM na makabaila, manyonyaji na mabeberu. Kwa sababu wameacha ile misingi ya awali ya chama hicho ya kupambana na rushwa, kutoruhusu matabaka baina ya wananchi. Hivyo ccm ya sasa ni tofauti na ccm asili. sina haja ya kulifafanua hilo maana kila mmoja wetu analifahamu.
Mwisho nasema.
OKTOBA 31 NDIYO HIYO IMEKUJA. USIFANYE MAKOSA MWANANCHI MWENZANGU,
CHAGUA KIONGOZI MAKINI,
CHAGUA KIONGOZI AMBAYE ANAIPENDA NCHI KWA DHATI KABISA,
CHAGUA KIONGOZI ANAYEHANGAISHWA NA UMASIKINI WETU,
CHAGUA KIONGOZI ANAYEPINGA RUSHWA NA UFISADI KWA DHATI,
CHAGUA DR. WILBROAD SLAA.
MWANA MAPINDUZI NA MZALENDO WA KWELI.
 
Mwacheni mzee achukue raslimali zake......Ah! Ah! CCM inawenyeweeeeeeee! (JK + Family, Roastham, Kimama, Makambako, EL wa Richmonduli, Rambaramba pesambili nk)
 
Kama taarifa hii ni kweli basi kazi ipo coz kila aliyeona hakutendewa sawa akaenda kung'oa yale yote aliyoyafanya, si yatabaki mahandaki ya hali ya juu.

I am sure mzee is not that bad jamani khaaa....
 
Its strange kwa Mzee Malechela kufanya kama inavyodaiwa,ila hiyo pump hatujui undani wake,ilitolewa kama mkopo walipaji deni wakashindwa ?au inamatatizo ya kiufundi ? Au matumizi mabaya au kaamua kuingoa tu.
 
Wapokea rushwa ya hiyo mashine hawakutimiza mkataba wao wa kumpitisha kura za maoni - Sio ajabu kama naye kachukua kilicho chake?
 
Mwl.Nyerere alikuwa ni mtu wa aina ya pekee sana...anaona mpaka kwenye roho ya mtu...watu wengi hawakumuelewa Mwalimu alipoelezea waziwazi kuwa huyu Malecele HAFAI KUWA KIONGOZI !!! Hawakumsikiliza na madhara yake wameyaona...na sasa wanakumbuka shuka kumekucha..na bado anawachapa kwa kofi la mwisho mwisho kwa kuwang'olea mashine ya maji..ni ishara tosha kuwa huyu kiongozi has never really cared from the bottom of his heart the well being of his wananchi...ilikuwa n sehemu ya KULA tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…