Malecela apongeza uimara wa CCM na Serikali zake kutumikia Watanzania

Ataka uzalendo zaidi sambamba na utekelezaji wa Ilani ya CCM

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuwa na moyo wa kizalendo na kujituma kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Akizungumza leo tarehe 5 Desemba 2024, baada ya kutembelewa nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Malecela alipongeza chama hicho kwa kuendelea kuonesha uongozi imara chini ya Mwenyekiti wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Malecela ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu (Bara), alisema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM unaendelea kwa kasi na umedhihirisha dhamira ya kweli ya chama hicho kuwatumikia Watanzania.

Alibainisha kuwa mafanikio ya Rais Dkt. Samia, hususan katika sekta za maendeleo ya miundombinu, afya, na elimu, yanapaswa kuwa chachu ya wanachama kuendeleza mshikamano na kuimarisha uongozi wa chama, ambacho kimejengwa juu ya misingi imara ya kutumikia watu.

“Wanachama wa CCM wanapaswa kuwa mfano bora wa uzalendo kwa wengine. Hili ni jukumu letu la kihistoria, ambalo tunapaswa kuliheshimu kwa vitendo,” alisema Malecela.

Kwa upande wake, Balozi Nchimbi alimshukuru Malecela kwa mchango wake wa mawazo na uzoefu unaoendelea kuwa hazina kubwa kwa Chama na Serikali.

Alisema viongozi wastaafu kama Malecela wamekuwa mstari wa mbele kutoa ushauri unaosaidia kuimarisha utendaji wa chama katika nyanja mbalimbali.

“Uzoefu wenu ni mwanga kwetu. Tunaendelea kuthamini mawazo yenu ambayo yamekuwa nguzo muhimu kwa chama na taifa kwa ujumla,” alisema Nchimbi.

Katika mazungumzo hayo, Malecela pia alitoa wito kwa wanachama wa CCM kuendeleza mshikamano na maadili ya chama, akisisitiza kuwa hiyo ni mojawapo ya misingi ya mafanikio ya CCM kwa zaidi ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

Aliwaasa viongozi wa sasa wa CCM kuendeleza kazi nzuri wanayoifanya huku wakizingatia misingi ya haki, uwazi, na uwajibikaji.

Alisema maadili ya uongozi bora yamekuwa kichocheo kikubwa cha imani ya wananchi kwa CCM.

“Huu ni wakati wa kuchapa kazi zaidi, kuhakikisha tunazidi kuimarisha maendeleo ya nchi yetu huku tukiheshimu dhamira kuu ya chama ya kuwatumikia wananchi,” alihitimisha Malecela.

#Ends

View attachment 3169948View attachment 3169949View attachment 3169950
Anatamani tu azikwe Kwa heshima.
 
Hivi hata anajua kweli kinachoendelea nchini sasa hivi? Inawezekana hata ameshau kuwa aliwahi kubadili dini akaitwa Jumanne ili apate support ya Iran kupata Urais wa Tanzania.Bure kabisa hili zee. Na pia hata hana kumbukumbu kuwa huyo aliyekaa naye hapo alituhumiwa kumtoa roho mwanawe Ipy katika harakati za kugombea uongozi wa Uvccm.
 
Malecela inabidi asifu tu, akiongea kama mwenzake Warioba atajibiwa nyodo, ataambiwa akae kimya ajilie pensheni yake taratibu
 
Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuwa na moyo wa kizalendo na kujituma kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Akizungumza leo tarehe 5 Desemba 2024, baada ya kutembelewa nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Malecela alipongeza chama hicho kwa kuendelea kuonesha uongozi imara chini ya Mwenyekiti wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Nchimbi, Nchimbi, Nchimbi..... Muacheni Mzee wa watu apumzike. msimfanye mzee wa watu mateka baada ya kumnyanyasa kimyakimya .... ana machungu yake moyoni huyu Mzee. Nendeni kwa Warioba au Matiku mpewe ukweli na hali halisi ya nchi.
 
Ataka uzalendo zaidi sambamba na utekelezaji wa Ilani ya CCM

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuwa na moyo wa kizalendo na kujituma kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Akizungumza leo tarehe 5 Desemba 2024, baada ya kutembelewa nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Malecela alipongeza chama hicho kwa kuendelea kuonesha uongozi imara chini ya Mwenyekiti wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Malecela ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu (Bara), alisema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM unaendelea kwa kasi na umedhihirisha dhamira ya kweli ya chama hicho kuwatumikia Watanzania.

Alibainisha kuwa mafanikio ya Rais Dkt. Samia, hususan katika sekta za maendeleo ya miundombinu, afya, na elimu, yanapaswa kuwa chachu ya wanachama kuendeleza mshikamano na kuimarisha uongozi wa chama, ambacho kimejengwa juu ya misingi imara ya kutumikia watu.

“Wanachama wa CCM wanapaswa kuwa mfano bora wa uzalendo kwa wengine. Hili ni jukumu letu la kihistoria, ambalo tunapaswa kuliheshimu kwa vitendo,” alisema Malecela.

Kwa upande wake, Balozi Nchimbi alimshukuru Malecela kwa mchango wake wa mawazo na uzoefu unaoendelea kuwa hazina kubwa kwa Chama na Serikali.

Alisema viongozi wastaafu kama Malecela wamekuwa mstari wa mbele kutoa ushauri unaosaidia kuimarisha utendaji wa chama katika nyanja mbalimbali.

“Uzoefu wenu ni mwanga kwetu. Tunaendelea kuthamini mawazo yenu ambayo yamekuwa nguzo muhimu kwa chama na taifa kwa ujumla,” alisema Nchimbi.

Katika mazungumzo hayo, Malecela pia alitoa wito kwa wanachama wa CCM kuendeleza mshikamano na maadili ya chama, akisisitiza kuwa hiyo ni mojawapo ya misingi ya mafanikio ya CCM kwa zaidi ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

Aliwaasa viongozi wa sasa wa CCM kuendeleza kazi nzuri wanayoifanya huku wakizingatia misingi ya haki, uwazi, na uwajibikaji.

Alisema maadili ya uongozi bora yamekuwa kichocheo kikubwa cha imani ya wananchi kwa CCM.

“Huu ni wakati wa kuchapa kazi zaidi, kuhakikisha tunazidi kuimarisha maendeleo ya nchi yetu huku tukiheshimu dhamira kuu ya chama ya kuwatumikia wananchi,” alihitimisha Malecela.

#Ends

View attachment 3169948View attachment 3169949View attachment 3169950
Malecela alifanya kitu gani cha maana kwa Watanzania......chawa kikongwe
 
Back
Top Bottom