Malecela amewataka wote wanaolumbana wakome mara moja kwani hayana tija na kwamba vyombo vya habari viendelee kufichua ufisadi badala ya kutumika kutukanana. Amekwepa sana kuzungumzia specific issue japo alipobanwa maswali kuhusu Dowans alisema kwamba hiyo ni sawa na kupiga bakora maiti ya farasi kwa kuwa suala hilo lilimalizwa na Bunge na kwamba kama kuna mwenye hoja tofauti alirudishe bungeni kwa utaratibu unaokubalika na si kulumbana kwenye vyombo vya habari. Akasema mambo ya CCM yamalizwe na CCM, ya Bunge yamalizwe bungeni, ya serikali ichukue hatua kwa yale yaliyo eneo lake, ili kila kitu kiwe na mwisho.. Akakumbushia wabunge waliowahi kutimuliwa chama na hatimaye ubunge wakiwamo Mwakitwange, Choga na Masha. Mengine baadaye, msimulizi yuko bize