Naomba mniwie radhi kwa kutoka nje ya maada kidogo, ninayojibu yametokana na Thread hii kwa mantiki hiyo ni kwamba nna stahili ya kuyajibia hapa.
Acha unafiki wewe mzozo!
Nani anasapoti kauli chafu?
Watu tunasonga mbele na wengine mnaanza unafiki wenu kama kawa!
Ndugu Yangu Jmushi,
Unaposema mtu aache unafiki ina maana ya kwamba yeye ni Mnafiki. Nashukuru kwa kunipatia 'Status' mpya hapa JF. Na nashukuru kwa kunitahadharisha ya kwamba niachane na Kauli chafu ila badala yake na nisonge mbele kulingana na taratibu zote za jukwaa.
Mbali na kuwa ni kioo cha Jamii, JF nadhani inaelimisha, fahamisha na ni njia ambayo Watanzania ambao tumejaaliwa kwa kufikiwa na Teknolojia ya mawasiliano ya Internet tunaimulika Serikali yetu, tukisifia mazuri na kukosoa mabaya.
Niliandika haya:
Ukiingia msituni na panga lako utaenda kufyeka miti ama? tukumbuke kwamba tunahamasishwa kutunza mazingira.
Vita ya safari hii ni vita ya Hoja, na Nguvu ya Hoja... ni vita ya kupigania Demokrasia, vita ya kuuacha ukweli ufahamike na kuweka ukweli wazi ili kila Mtanzania afahamu thamani ya Utu na Utanzania wake.
Vita ambayo tutashinda siku ile ambapo tutaamka na kupiga kura ambayo itatuhakikishia kwamba tunajiongoza wenyewe.... na tutakapoacha kupiga kura ya kula.
naomba unisaidie kwa kunifahamisha ni nini Unafiki wangu katika hilo hapo juu. Utakuwa umenisaidia kwa kunielimisha vya kutosha.
Jambo la pili kwa kweli nafahamu ya kwamba ni watu wengi sana wamekuwa wanaliongelea, ni pale ambapo mtu unakuwa unaingia na kuanza kuchangia katika maada kwa kushambulia bila hata kujua unaandika nini na unapinga nini na kukubaliana na nini. Hata Bendera nazo hufuata upepo; sasa wewe sijajua kama unaandika ili kuongeza idadi ya
'Posts' ulizonazo ama kuridhisha macho yako. Hii ni moja kwa moja kwa Ndugu Yangu JMushi.
JMUSHI
Msimamo wangu kuwa mafisadi wakamatwe ndio msimamo wa wananchi!
sasa nyie mnaotaka kuni attack personally mtaumbuka!
Nakufahamu gaijin!
Najua una ushabiki wa watu flani flani!
Mimi sina!
Niko hapa kwa wakati wa Mungu!
Nakata issues!
Ningekuwa na haja ningekuwa nawapigia simu hao vigogo kama wengine wafanyavyo!
Sina haja hiyo kwasababu nimezisoma RIPOTI ZOTE NA SASA UKWELI UMWENIWEKA HURU!
MAFISADI WAKAMATWE MARA MOJA!
[QOUTE]
Not me!
Mi nachambua tu hapa!
Wapi hapo umeona nimemsapoti politician wakati huu?
Hapa tunakata issue!
Kama ningejali pundits nad cynists..Ningetangaza kujitoa jf kama Mchambuzi..Halafu unadhani sura ya mchezo ingekuwa hivi?
Jf ni kioo cha jamii na viongozi wa kambi zote wako hapa wakati tunakata issue!
Upande wa ccm ukishinda kwa hoja...SAWA WAPEWE NCHI!
Upande wa wazalendo ukishinda pia wapewe nchi kwa niaba ya watanzania!
[/QUOTE]
Nyie mnaotaka kurudisha hoja kuwa Jmushi mna lenu!
Watu wamesharudi kwenye hoja lakini mnataka kuwarudisha kwenye malumbano!
Wana jf msikubali!
Endeleeni hoja mimi niko kando!
Naomba nimshukuru huyu Member (Samahani nilisahau ku-quote jina) nadhani Jmushi angekuwa anasoma kila kitu na kupata mwelekeo wa mjadala asingekuwa anatuletea hizo GIGO (Garbage In Garbage Out).
Hoja muhimu kama hii, unakuta almost 4 pages ni ubishani wa jmushi1 kuhusu mambo ambayo hayana mtiririko wa hoja, sasa hii inatupotezea muda mrefu sana kusoma topics nyingi humu ndani kwani mtu unatumia unnecessary time kudeal na hiyo GIGO ya Jmushi1.
Nothing can be done wazee au ni mimi mwenyewe ndio napata hii shida????
Heshima Mbele.