Malengo maovu ya wakubwa wa dunia

Malengo maovu ya wakubwa wa dunia

Teleskopu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2017
Posts
702
Reaction score
767
Dunia hii ina watu wanaoongoza mambo yote makubwa, kama vile uchumi, elimu, majeshi, sayansi, nk.

Kwa bahati mbaya sana, watu hawa wana malengo maovu mno, licha ya kuwa wao ni kikundi kidogo sana. Lakini baya zaidi asilimia zaidi ya 90 ya wanadamu hawana habari na kile kinachoendelea. Wakubwa hawa wanawaita hawa waliolala sheeple au goim.

Ili hawa sheeple waendelee kulala usingizi wa pono, na kuwaacha wakubwa wakiendelea kukamilisha mipango yao, wamewekewa mambo ya kipuzi ya kuwa-keep busy, kama filamu, mipira, muziki, vita kati ya nchi na nchi au dini na dini, nk, nk.

Malengo ya wakubwa hawa ni pamoja na:
  • Kupunguza SANA idadi ya wanadamu
  • Kuwa na totalitarian government kwenye dunia yote, yaani utawala wa udikteta, tena mkali.
  • Kumtawala KILA MTU kwa kumwamulia cha kufanya, cha kula, pa kwenda, cha kuabudu na hata cha kufikiri.
  • Kumiliki rasilimali ZOTE duniani – iwe ni madini, maji, misitu, nk.
Ifuatayo ni video iliyoandaliwa na World Economic Forum ambayo ukiisikiliza ni kama kichaa anaongea. Lakini hayo ndiyo yanayoujia ulimwengu. Hawa watu wamejipanga kwa miaka ipatayo 300 sasa.

Video hii inasema​
Dunia inabadilika haraka.​
Idadi ya watu inazidi kuongezeka.​
Lakini tunaweza kushughulikia hilo.​
Hadi kufikia 2030 halitakuwa tatizo tena.​
Kwa msaada wa virusi vya kutengeneza
Na mashambulizi ya kiuchumi yanayolenga shabaha kwa usahihi (precision attacks)​
tunaweza kushughulikia tatizo la binadamu​
Wale mtakaobakia
Mtakuwa mkilindwa chini ya uangalizi​
Mtaishi kwenye vijumba vidogo​
Nyama si nzuri kwa afya​
Mtakula wadudu​
Hamtamiliki chochote na mtakuwa na furaha.​
…………
Hapa tunaona mambo kadhaa ya msingi:
  • Wanadamu wengi kwao ni tatizo.
  • Tatizo hilo mwisho ni mwaka 2030. Naamini umeshasikia kuhusu Agenda 2030.
  • Yanakuja mashambulizi ya kiuchumi, mfano matetemeko, mafuriko, ukame, nk – YA KUTENGENEZA!!! Nayo ni precision attacks, yaani wakitaka tetemeko lipige Dar es Salaam na kufumuafumua bandari mnayotegemea, wanaweza – watu wamesha-advance kiasi hicho. Ni sisi tu tunaoshinda kuangalia mpira na filamu ndio tunaweza kubisha mambo hayo.
  • Kuna watakaobakia – yaani wengine wataondoshwa.
………….
MASWALI YA KUJIULIZA
  • Watawezaje kupunguza wanadamu hadi wasiwe tena tatizo kama wanavyotuona?
  • Watawezaje kumtawala kila mwanadamu atakayebaki duniani kote?
  • Video inaposema TUNA... ni akina nani hao?
Kesho nitafafanua namna bill gate anavyoingia naye kwenye suala hili.
………….
Dunia inaswagwa kupelekwa mahali fulani.
Na wengi wamelala usingizi fofofo.
Hawana habari.
The world is not what you think it is!
Connect the dots.
.......
Pamoja na yote uyafanyayo ndugu yangu - USIMSAHAU MUNGU.
Dunia uliyoijua tangu uzaliwe IMEISHA. Tumo kwenye enzi nyingine kabisa sasa.
 
Stor za abunuasi, kuitawala dunia ni kazi sana ingawa wanajitahid. Unajua kwa nini?? Mataifs yenye nguvu, elimu na sayansi bora yanazid kuongezeka hivyo resistance itakuwa kubwa zaidi na zaidi
 
Stor za abunuasi, kuitawala dunia ni kazi sana ingawa wanajitahid. Unajua kwa nini?? Mataifs yenye nguvu, elimu na sayansi bora yanazid kuongezeka hivyo resistance itakuwa kubwa zaidi na zaidi
Sote tunaomba iwe hivyo mkuu. Tatizo ni moja. Viongozi karibu wote duniani ni wanachama wa makundi ya siri yanayoongoza mambo haya. Maana hii si mipango ya serikali. Serikali zinatumiwa tu kama chambo
 
Aiseee.ngoja niongeze kula matunda mengi zaidi kimasiara..kabla hawajatusepesha hiyo 2030
 
Yap Usemayo ni kweli tupu na hata huu ugonjwa wa ukimwi na corona na chanjo zake na ARV ni hao hao na bado kuna mengi yanakuja tukae kwa kutulia
 
Hao wanaofanya hivyo hawafi??
Means pia kuna watakao zaliwa wataendeleza??
 
Hao wanaofanya hivyo hawafi??
Means pia kuna watakao zaliwa wataendeleza??
Watakufa lakini hawajali walishajitoa kumwabudu shetani na kufaidi mali za dunia kwa kitambo
 
Watakufa lakini hawajali walishajitoa kumwabudu shetani na kufaidi mali za dunia kwa kitambo
Kwahiyo basi,anefanya yote haya ni shetani,hawa wengine ni vibaraka tu?
 
Back
Top Bottom