Malengo ya Elimu ya Tanzania ni mawili, 1. Tunasoma ili tufaulu mitihani, 2. Tunasoma ili tuajiriwe. Njoo ubishe kwa hoja

Malengo ya Elimu ya Tanzania ni mawili, 1. Tunasoma ili tufaulu mitihani, 2. Tunasoma ili tuajiriwe. Njoo ubishe kwa hoja

Hivi serikali ilishawahi kujiuliza maswali ya kielimu kuhusu raia wake wengi wanaohitimu ngazi mbalimbali za elimu huwa wanaishia wapi ikiwa lengo la kusoma ni kufaulu mtihani na kuajiriwa? Ianzie na hao wanaofeli wanaishia wapi? Au inafikiri ndio hawa bodaboda, wamachinga na wengine wengi wa aina hii? Serikali ina mkakati gani kuboresha stadi za kazi kwa raia ambao si wanafunzi wa vyuo na shule? Au wakimaliza ngazi za elimu wao huchukua wafanyakazi wake na hao wanaobaki wapotelee kusikojulikana wakitafuta maisha bora? Elimu haina serikali inatakiwa iwe na mipango na programu nyingi za kukuza na kuendeleza stadi za kazi kwa raia wake nje na mfumo rasmi wa elimu
 
Halafu kama bodaboda ni ajira tuone mtoto mmoja wa mfanyaabiashara au mwanasiasa mkubwa aajiriwe huko kwenye bodaboda
 
Mabdadiliko ya elimu yataletwa na waliofeli mitihani wakakosa kuajiriwa huku wakiwa na maarifa ya kutosha sawa na waliofaulu na kupata ajira. Hawa walioko kwenye ajira hawawezi kuleta mapinduzi ya kielimu hata kama ni watunga sera kwa kuwa wananufaika na mfumo uliowapa ajira hawana jeuri ya kuuasi na kuusaliti. Yaani hawajui maisha ya ku hursle na straggle for exstance/fittest. Mtu ana ajira hawezi kuona mapungufu ya elimu anaona mambo yako sawa. waliopata elimu wakaishia kukatishwa ndoto zao za kufikia mafanikio ya juu kielimu, mwanafunzi unakaririshwa makemistri, maboyolojia na mafiziksi mwisho unatangaziwa umefeli huruhusiwi hata kuuza kidonge cha panado, hurusiwi kucheza makidakida na kuimba a e i o, u. Utaambiwa lete cheti. Ina maana hawatambui zile asilimia za maksi alizopata mwanafunzi, yaani wanamfutia maarifa yote aliyofundishwa tangu msingi hadi chuoni. Ni upuuzi mtupu kudhani waliofeli mitihani kichwani hawana akili. Tena ogopa mtu uliyempa elimu nusu au robo, bora umpe elimu iliyokamilika.
 
tunasoma ili tufaulu ndo maana anaepata point 7 o level ana akili wakati alikesha miaka minne akisoma usiku mzima saa 7 saa 8 usiku anarudi kila siku kwahiyo bongo ukitaka mwanao aonekane msomi na mwenye akili akariri tu vitabu na maandishi kwa namna yoyote ile atapata sifa sana RIP mifumo yetu ya elimu
 
Back
Top Bottom