Mabdadiliko ya elimu yataletwa na waliofeli mitihani wakakosa kuajiriwa huku wakiwa na maarifa ya kutosha sawa na waliofaulu na kupata ajira. Hawa walioko kwenye ajira hawawezi kuleta mapinduzi ya kielimu hata kama ni watunga sera kwa kuwa wananufaika na mfumo uliowapa ajira hawana jeuri ya kuuasi na kuusaliti. Yaani hawajui maisha ya ku hursle na straggle for exstance/fittest. Mtu ana ajira hawezi kuona mapungufu ya elimu anaona mambo yako sawa. waliopata elimu wakaishia kukatishwa ndoto zao za kufikia mafanikio ya juu kielimu, mwanafunzi unakaririshwa makemistri, maboyolojia na mafiziksi mwisho unatangaziwa umefeli huruhusiwi hata kuuza kidonge cha panado, hurusiwi kucheza makidakida na kuimba a e i o, u. Utaambiwa lete cheti. Ina maana hawatambui zile asilimia za maksi alizopata mwanafunzi, yaani wanamfutia maarifa yote aliyofundishwa tangu msingi hadi chuoni. Ni upuuzi mtupu kudhani waliofeli mitihani kichwani hawana akili. Tena ogopa mtu uliyempa elimu nusu au robo, bora umpe elimu iliyokamilika.