Ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba hili tatizo linaendelea kukua siku hadi siku. Kuna mwanachama mmoja alilalamika majuzi kuhusu huu mtindo ambao ofisini kwake walivunja hadi choo!
Haya mapenzi yako ya aina mbili:
1. Mkubwa kumlazimisha mdogo kwa lengo la aidha kumpa ajira, kumpandisha cheo, au kumuidhinishia safari nje ya kituo.
2. Mdogo kujipendekeza kwa bosi kwa malengo hayohayo.
Namba moja ndio inatumika zaidi na mara nyingine ngono zinafanyika humohumo ofisini!
Kwa mfumo huu tija katika kazi haiwezi kuwepo. Sijui sheria za kazi zinasemaje kuhusu huu unyanyasaji wa kijinsia.