Malengo ya mapenzi ofisini

Malengo ya mapenzi ofisini

pembe

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
2,150
Reaction score
717
Ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba hili tatizo linaendelea kukua siku hadi siku. Kuna mwanachama mmoja alilalamika majuzi kuhusu huu mtindo ambao ofisini kwake walivunja hadi choo!

Haya mapenzi yako ya aina mbili:
1. Mkubwa kumlazimisha mdogo kwa lengo la aidha kumpa ajira, kumpandisha cheo, au kumuidhinishia safari nje ya kituo.
2. Mdogo kujipendekeza kwa bosi kwa malengo hayohayo.

Namba moja ndio inatumika zaidi na mara nyingine ngono zinafanyika humohumo ofisini!
Kwa mfumo huu tija katika kazi haiwezi kuwepo. Sijui sheria za kazi zinasemaje kuhusu huu unyanyasaji wa kijinsia.
 
View attachment 111392View attachment 111392 View attachment 111394

kusema ukweli, ngono ya maofisini kama wewe ni boss, kama umelazimisha, ni kosa la ubakaji na likithibitika linaweza kumpelekea mtu miaka si chini ya thelathini. siku hizi kuna simu na hadi saa zinaweza kurekodi jambo bila mtu kujua. kuna saa fulani hivi inavaliwa mkononi tu, inauzwa garama sana laki si chini ya nane, ina gb kubwa tu unaweza kurekodi kitu bila mtu kujua. ushahidi ukiwepo mtu kama huyo akirekodiwa itasaidia.

pia, kwa ngono ambazo wadada wanajipendekeza, huo ni uzinzi na uasherati ambao Mungu atawahukumia adhabu.

bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI kupata kitabu kinachoongelea ngono za ofisini kama ni ubakaji na mambo mengine mengi.
 
Kinachoshangaza hivi vitendo vinafanyika lakini sijaskia mtu ameshitakiwa ina maana kuna namna ya kwamba liwalo na liwe? Au ni kama hii orodha ya watu wa madawa ya kulevya? Ile kamati ya maadili ingeitisha maoni maofisini wangepata ripoti ya ajabu!
 
Back
Top Bottom