Malengo ya Milenia (MDGs): Tanzania tu wapi?

Malengo ya Milenia (MDGs): Tanzania tu wapi?

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2012
Posts
3,598
Reaction score
1,544
Salaam wana JF,

Ikiwa imebaki miaka mitatu kufika mwaka 2015, yaani ukomo wa muda Umoja wa Mataifa(UN) iliyotoa kwa nchi 193 wanachama(miaka 15 toka mwaka 2000), malengo kadha wa kadha(Malengo ya Milenia) katika kuendeleza, kuelimisha, kupunguza utegemezi na kuendeleza ushirikiano wa nchi hizo.

Na kupitia mashirika mbali mbali ya Umoja huo mfano WHO, UNDP, n.k kupitia malengo hayo kwa nchi wanachama yalikuwa/ni haya yafuatayo;

1. Kupunguza na kuondoa ufukara na Njaa.
-Kufanikisha angalau nusu kwa uwiano wa wale wanaoishi chini ya dola moja ya Kimarekani.
-Kupunguza angalau nusu ya watu wenye njaa.


2. Kufanikisha Elimu ya Shule ya msingi kwa wote.
-Uandikishwaji wa watoto waliofikisha umri wa kwenda shule
-Wanaoandikishwa kumaliza wote.
-Kuwawezesha wafaulu na kuendelea na elimu ya Sekondari.


3. Kuhamasisha usawa kijinsia na Kuwawezesha wanawake.

-Kuondoa upungufu huo kwa kuweka usawa kijinsia katika nyanja za elimu, siasa
-Kuwawezesha wanawake, katika nafasi za Bunge kuweka usawa.


4. Kupunguza vifo vya watoto.
- Watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano.
-Watoto walio na umri chini ya mwaka mmoja.
-Uwiano wa watoto walio na umri chini ya mwaka mmoja na wanaopata kinga dhidi ya Surua.


5.Kuboresha Afya ya kina mama wajawazito.
-Kupunguza vifo vya kina mama wajawazito(MMR)
-Kuongeza vituo vya kliniki za wajawazito.
-Kufikisha lengo la Uzazi wa Mpango.

6. Kukabiliana na magonjwa kama UKIMWI,Malaria, Kifua Kikuu na magonjwa mengineyo.
-Kutumia kinga ya kondomu kwa umri hatarishi.
-Kuwezesha kupata madawa ya ARV kwa waathirika.
-Kuwezesha upimwaji, kupata tiba sahihi ya Malaria.
-Kuhakikisha utumiaji wa dawa za Kifua kikuu kwa uangalizi wa mhudumu wa Afya(DOTS).


7. Kuhakikisha utunzwaji, uboreshwaji wa mazingira.
-Usawa katika uwiano wa upatikanaji wa maji safi, kati ya maeneo ya mjini na vijijini.
-Kupunguza matumizi mabaya yenye kuharibu utanda wa Ozone(Ozone layer)
-Kutunza, kulinda viumbe wa nchi kavu, angani na majini wanaotaka kupungua.


8. Kuendeleza ushirikiano wa kimataifa wa nchi mbalimbali.
-Kusaidia/Kupunguza kwa deni katika nchi zinazoendelea.
-Soko la usawa kwa bidhaa mbalimbali.
-Kuongeza misaada kwa nchi zinazoendelea.
-Kuhamasisha utumiaji wa teknolojia na nyenzo zake.


Ikiwa ni malengo nane yenye kuwa na vipengele mbalimbali(tajwa hapo juu ikiwa ni BAADHI tu)..Tujiulize,
-Sisi kama Nchi ya Tanzania Tumefika wapi?
-Kama mmoja mmoja(yaani mwana JF) tumefanya jitihada gani kutekeleza haya?
-Ni kwa sehemu gani tumefanya vizuri, tunapostahili pongezi na kuimarishana(kama Taifa, kama mmoja mmoja)
-Ni kwa sehemu gani tunasusua na tunahitaji kukumbushana, kuelekezana?

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom