Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 270
- 362
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuongeza ukuwaji wa uchumi na kudhibiti mfumuko wa bei kati ya 3% - 5% kwa 2022, licha ya kuwa na matatizo mengi nje ya nchi kama vita vya Ukraine na Urusi na kupanda kwa bidhaa kwenye soko la dunia ambayo yanaweza kudhuru ukuwaji wa uchumi wetu na kupelekea mfumuko wa bei, iko mikakati thabiti iliyowekwa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kutunusuru.
- Kazi kubwa ya kwanza ni kudhibiti mfumuko wa bei pamoja na kuimarisha ukuwaji wa uchumi na uzalishaji wa ndani.
- BoT iko macho kutazama sababu zote kutoka nje ya nchi ambazo zinaweza kudhuru uchumi wetu. Na sera yetu ya fedha inaweza kubadilika kila wakati kulingana na mwenendo wa dunia.
- BoT kwa sasa inatazama namna ya kuongeza hifadhi ya fedha za kigeni kwa 11.4%
- BoT itaongeza fedha za kutosha kwenye mzunguko kwa 10.3%, kupunguza viwango vya riba kwenye mabenki watu wakope kwa wingi ili kupunguza ugumu wa maisha.
- BoT itaimarisha huduma za kifedha kwa mabenki ili kuzifanya benki zikopeshe zaidi sekta binafsi kwa 10.7%. Sekta binafsi zikipata fedha huchochea uzalishaji na ajira kwa wingi nchini.