Malengo yangu 2023 yasipotimia yanabaki ni malengo yangu ya maisha

Malengo yangu 2023 yasipotimia yanabaki ni malengo yangu ya maisha

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
‭Kwa mwaka 2023 nimejiwekea malengo yangu haya;
  1. Kununua kiwanja cha biashara (nina viwanja na nyumba kwa ajili ya makazi) 2023 nimeupa rasmi ni mwaka wa mandalizi ya kuongeza biashara nyingine hivyo ntapambana ninunue uwanja either for guest house au kiwanda kidogo, sijui itakuwa biashara gani muhimu nipate ardhi kwa ajili ya biashara.
  2. Kununua tena shamba (huu ni utaratibu wangu kila mwaka lazima niongeze shamba, haijalishi ukubwa gani muhimu liwe shamba ninaloweza kulima).
  3. Kukuza mtaji wangu wa biashara kwa kujikita sana kwenye uzalishaji wa mazao na ufugaji (nimejifunza sana kuzalisha mwenyewe mazao yako na kupeleka sokoni inalipa zaidi kuliko kununua kwa wakulima na kuuza tu.
  4. Kuacha kabisa kufanya biashara hapa Tanzania (mfumo wa biashara hapa kwetu unahitaji uwe mtoa rushwa kidogo, mshirikina kwa mbali, visa visa na watu hivi ni vitu sipendi mno kwenye maisha yangu.
  5. Kuoa rasmi (niishi na mwanamke ndani kwangu sio hii kila mtu anaishi kivyake), hili linahitaji sana maombi, maana kila mwaka naweka lengo hili ila nashindwa hadi nimetimiza miaka 35 na hamu ya ndoa sina kabisaaa.
Karibu nawe weka malengo yako hapa chini tuwe tunakumbushana‬.

NB: Nisipotimiza kwa mwaka 2023 haya hapo juu, sitobadili kabisa malengo huwa naamini kufanikisha nilichokipanga haijalishi inaweza nichukua muda gani.
 
‭kwa mwaka 2023 nimejiwekea malengo yangu haya 1. kununua kiwanja cha biashara ( nina viwanja na nyumba kwa ajili ya makazi ) 2023 nimeupa rasmi ni mwaka wa mandalizi ya kuongeza biashara nyingine hivyo ntapambana ninunue uwanja either for guest house au kiwanda kidogo ,sijui itakuwa biashara gani muhimu nipate ardhi kwa ajili ya biashara 2 . kununua tena shamba(huu ni utaratibu wangu kila mwaka lazima niongeze shamba , haijalishi ukubwa gani muhimu liwe shamba ninaloweza kulima .3.kukuza mtaji wangu wa biashara kwa kujikita sana kwenye uzalishaji wa mazao na ufugaji ( nimejifunza sana kuzalisha mwenyewe mazao yako na kupeleka sokoni inalipa zaidi kuliko kununua kwa wakulima na kuuza tu 4. kuacha kabisa kufanya biashara hapa Tanzania ( mfumo wa biashara hapa kwetu unahitaji uwe mtoa rushwa kidogo,mshirikina kwa mbali , visa visa na watu hivi ni vitu sipendi mno kwenye maisha yangu 5. kuoa rasmi ( niishi na mwanamke ndani kwangu sio hii kila mtu anaishi kivyake, hili linahitaji sana maombi, maana kila mwaka naweka lengo hili ila nashindwa hadi nimetimiza miaka 35 na hamu ya ndoa sina kabisaaa, karibu nawe weka malengo yako hapa chini tuwe tunakumbushana‬, nb nisipotimiza kwa mwaka 2023 haya hapo juu , sitobadili kabisa malengo huwa naamini kufanikisha nilichokipanga haijalishi inawezA nichukua muda gani
Naunga mkono mipango yako yote kasoro hilo la kuoa.

Alafu si tulikubaliana ili ufankiwe inabidi uwe na siri?? Mbna ww umefichua siri ya mipango yako?
 
Back
Top Bottom