Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa

Ni sawa lakini usipooa utaolewa.
 
wanaume tunamuwakilisha Mungu duniani. sasa tuna declare kushindwa jukumu letu, ni aibu sana

Mwanzo 3:16​

Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.

Mwanzo 2:18​

BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
 
Tunakataa pepo la kuoa kwa nguvu zote lishindwe kwa maana wanawake wanaingia kwenye ndoa kama kupe, ambao si wana wa Mungu, hawana imani ya kweli na msukumo wa kweli na Nia na madhumuni thabiti ya kumuishi Mungu kwa muktadha wa ndoa, haiwezekani tuache maisha mazuri tukubali kuchinjwa na hawa kupe.

Kuna haja ya kuja na mafundisho ya kuwajuza watu ndoa ya kweli ifaayo machoni pa Bwana Mungu wetu inapaswa kuwa namna gani, namna ya kumshirikisha Mungu awezeshe ndoa peke zenye kumpendeza yeye katika kweli.

Kataa ndoa fake bila kuoa ni heri zaidi kuliko kuishi maisha ndoa fake.

Lakini kwa haya mapanya na manyoka ya kike, nakazia ndoa hapana.
 
Kataa ndoa uwe salama kiakili

Kataa ndoa uishi maisha marefu yasiyo na bughudha

Kataa ndoa uwe huru kimwili, kiakili na kiroho

Kataa ndoa uwe mtazamaji wa matatizo ya watu ☺️☺️

Kataa ndoa ujue kutofautisha kati ya 6 na 9


Ila kwakweli ndugu yenu mimi nimeoa na nina watoto wawili
 
Kamleee hamna tatizo ila wewe labda kama ni mama wa nyumbani ila wakiume una mambo mengi kachukue mtoto wa miaka 3 Kam utaweza kumlea.
Kwani hakuna nanies? Kwani hata huyo mwanamke ukimoa atakuwa anashinda na mtoto masaa 24 au?
 
Hizi hofu ni madhaifu na mapungufu katika ndoa.. Ukiona mwanamke anachepuka kisababishi kwa asilimia 90 ni mwanaume nina mifano ya kutosha

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
Kizazi kilichokengeuka, wanaume vichwa vipo race kama gari ya langalanga wanawake nao madishi yameyumba kama yamepigwa na cyclone.

Hiyo ndoa hata ikifungwa ndani ya miezi kadhaa walishaachana.

Ndio maana wanaona haina haja ya kuoa.
 
Atafute mwenyewe kwa vigezo vyake mkuu.

Mambo ya kutafutiana tena!

Aweza kuletewa mwanamke mwenye vigezo alivyoridhika navyo mama yake, lakini yeye visimridhishe.

Kwenye kuoa tunaanzaga kwanza na sura halafu memgine ndiyo yanayofuata, ndiyo maana husemwa: "uzuri wa mwanamke upo kwenye jicho la muoaji".

Kuoa ni sawa na kujenga nyumba ya makazi.

Lazima kabla ya kujenga, uchague "site" ya eneo unalolipenda, chora ramani kutokana na utashi wa nyumba ambavyo unataka iwe.

Ukinunua nyumba yoyote popote, waweza kukinaishwa kuishi kwayo baada ya muda mfupi sana na ukaamua kuiuza.
Huo ni mfano nimetolea.

Mengine namna ulivyoshauri nakuunga mkono 100%.
 
Kuharibika kwa utamu wa ndoa mpaka kufikia vijana wengi wa kiume kuanza kuona ni upuuzi, kulianzia hapa "UKIMUELIMISHA MWANAMKE UMEELIMISHA JAMII NZIMA" na hatimae jamii imeelimika vya kutosha juu ya hao wanawake, pia kingine ni hapa "HAKI SAWA" haka notion kapo kwenye akili za wanawake na huwa wanaingia nako kwnye ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…