Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa

Katka vitu vinasababisha ndoa kuto dumu ni pamoja na tabia za wanaume kupenda aina flani ya wanawake ambao hawaendani nao kitabia, kama wewe ni mlevi oa mlevi mwenzio usitafute mchamungu hautadumu, nae kama mzinzi oa mzinz mwenzio we ukipita huku ye kapita kule ila ukioa alietulia akiona wew unachepuka hata vumilia, angalia tabia yako tafuta unaendana nae ili kama kwenye tungi muende wote.
 
1. Kwani kuna tatizo/madhara mtu asipo oa au olewa ?

2. Kwani ndoa ni swala la lazima au hiari ?

3. Umuhimu wa ndoa upo wapi ambao hawaja oa wana ukosa ?

Naomba mleta mada unipatie majawabu ya hayo maswali matatu ya mwanzo.
 
Malezi yanachangia na wengine n kuiga mkumbo ,kama watu wanavyojisifia mambo ya kijinga kama three some na mengne.ila sababu wamekataa uwepo wa maarifa ya mungu nae uwaacha wapotee,kuna njia ionekayo njema machoni pa mtu ila ni ya upotevu.
 
Ndoa ingekuwa ni kitu chema hivyo usingewabeza ambao hawataki kuoa. Nyie kuleni raha tuacheni sisi ambao hatujaoa tuendelee kuteseka. Au sio?
Wasiooa ndio wanawabeza waliooa kuwa wanateseka. Hoja yao kubwa ndio hiyo yakuogopa kuteseka wanaogopa kuumizwa hisia zao. sasa huo ni utoto kuogopa kivuli chako mwenyewe
 
Hapo umeongea ukweli.
Wanawake wameelimika na imekuwa ni changamoto kwa vijana wa kiume wasio jiamini.
The future is Female.
 
1. Kwani kuna tatizo/madhara mtu asipo oa au olewa ?

2. Kwani ndoa ni swala la lazima au hiari ?

3. Umuhimu wa ndoa upo wapi ambao hawaja oa wana ukosa ?

Naomba mleta mada unipatie majawabu ya hayo maswali matatu ya mwanzo.
Nitakujibu kwa weledi
Kichwa cha habari kinasema malezi duni na utandawazi
Msingi wa kwanza kabisa wa malezi bora ya mtoto ni familia yenye upendo, yenye kujali na yenye ushirikiano na mipaka

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
Hakuna madhara yoyote mkuu, pia ndoa ni suala la hiari hilo lipo wazi.
Mtu aoe au kuolewa kwa matakwa yake bila kulazimishwa.

Asiyetaka kuoa ama kuolewa asishawishi wengine kufanya hivyo. Hii kampeni inawaharibu vijana wenye akili ndogo...tuwaache wafanye maamuzi yao binafsi.
 
Ulicho sema ni kweli. Hizi kampeni za "kataa ndoa" sioni kama zina maana kwa upande wangu ila wenda zina maana kubwa kwa wale wanazo zitangaza kila uchwao na wana sababu zao za msingi za kufanya hivyo.
 
Nitakujibu kwa weledi
Kichwa cha habari kinasema malezi duni na utandawazi
Msingi wa kwanza kabisa wa malezi bora ya mtoto ni familia yenye upendo, yenye kujali na yenye ushirikiano na mipaka

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
Mkuu ningependa uni tenganishie majawabu kama ambavyo maswali yame kaa katika mtiririko, hivi ulivyo jibu hakuna nilicho elewa kutokana misingi ya maswali ulivyo kuwa.
 
Ulicho sema ni kweli. Hizi kampeni za "kataa ndoa" sioni kama zina maana kwa upande wangu ila wenda zina maana kubwa kwa wale wanazo zitangaza kila uchwao na wana sababu zao za msingi za kufanya hivyo.
Wanaokomalia hii kampeni wengi ndo hao hao wanaofanya kampeni ya mapenzi ya jinsia moja., na wengine ni kukwepa majukumu.
Hatukatai kwamba ndoa zina matatizo mengi tu lakini haimaanishi ya kwamba kila ndoa ina matatizo, wapo wanaoishi vizuri bila tatizo.
Na wanaposema tukatae ndoa ina maana watu waache kuzaliana? Au ndo wanafurahia ongezeka la single mothers?
 
Tunataka kuunda Taifa gani bila ndoa?
~ Ndoa ndio chanzo cha familia.
~ Ndoa ni dalili njema ya ukomavu wa akili.
~ Ndoa ni msingi wa uwajibikaji kujali, amani, furaha na upendo.
~ Ndoa ni future, bila ndoa future haina maana sana.
Ilivyo hivi sasa ni kwamba maisha yamekuwa magumu na uwezekano wa kustawisha ndoa ni mgumu sana, unaweza kuwa na ndoa lakini kama huna uhakika wa kipato basi uwezekano wa mke kuwa wa kijiji kizima ni mkubwa.

Ustawi wa ndoa unaanza na mfumo wa maisha katika nchi husika, vinginevyo hata ingehubiriwa kila kona vijana waoe kama mifumo imeyumba tusitegemee kustawi kwa ndoa, narejea takwimu kwamba Dar ina ndoa 300 zinazovunjika kila mwezi sawa na ndoa 10 kwa siku.

Kabla hatujawalaumu wanao kampenia kutokuoa tutazame ni wapi kama taifa tumekosea ili marekebisho yafanyike kwa kuzingatia makosa yaliyofanywa katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, mtaa, kijiji, Kata, Wilaya Mkoa na hata Taifa, Imani za dini, itikadi za kisiasa nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…