Nina kijana wangu ana soma form one, maendeleo yake ni mazuri sana kwani ameweza kuwa wa 2 kati ya watoto 140. Sasa ili kumpa motisha nilimwambia nitampeleka out siku ya mwisho kabla hajaenda shule na marafiki zake, nilipanga kumpeleka Best Bite au steers kabla hajaenda shule kesho Jumamosi. Lakini kuna tabia moja amefanya imeniudhi sana, msichana wa kazi alikuwa anafanya usafi bahati mbaya katupa kitambaa chake cha kufutia miwani. Ameanza kumtukana huyo msichana, kachukua simu yake na kumwambia hata mpa mpaka amtafutie kitambaa chake.
Sasa nauliza ili kumrekebisha hiyo tabia mbaya, nisimpeleke huko nilikomwaahidi kwaajili ya kumpa motisha au nifanyeje? kwani sipendi awe na tabia hiyo na pia ajifunze uvumilivu kuishi na watu.