Malezi ya kijana msaada

Mkuu mpeleke huko kwenye ahadi yake, na utumie huo muda mkiwa huko kumwambia.
hapana jamani. Huko anataka akamfurahishe mtoto, kuanza kukumbushia kesi za nyumbani kutaharibu lengo zima la mtoko.

Halafu anataka awapeleke na rafiki zake. Haitokuwa vizuri kuongelea hayo mambo ya kifamilia mbele ya rafiki zake.
 
Ulitakiwa kumkanya hapo hapo,kuchelewa kwako ni dalili ya woga,akizoea hiyo tabia ataota mapembe.Juu ya yote mtimizie ahadi yake.
 
Jamani mbona nimesema sijaonana nae, na wakati anafanya kitendo hicho mimi nipo kibaruani , hapa nimepigiwa simu tu sijaenda hata nyumbani
 

Ni bora nikueleweshe ktk hili la tabia. Kiukweli mtu hajifunzi/hafunzwi tabia ukubwani.Mtoto hujifunza tabia mbalimbali toka akiwa na Umri 0 hadi miaka 6.Halafu huwa hivi cha kwanza kuingia ktk ubongo huwa cha mwisho kutoka,sasa yale matendo au tabia ambazo atazionesha afikiapo umri wa miaka 10-18 ni MATOKEO YA MALEZI NA MAKUZI YAKO/YENU toka alipokuwa na Umri 0. Nakushauri umwelekeze kwa utulivu wa hali ya juu huwenda akakuelewa na akapunguza dharau na hasira, ila hiyo ndio tabia yake hataiacha jitahidi kumvumilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…