Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
...'insurance' tu hiyo. Hata mimi nilijiwahi na mapeema. Ya nini kusubiria umalize madarasa ilhali elimu haina mwisho? Hakikisha last born wako yupo chuo kikuu kabla hujastaafu, otherwise 'kiinua mgongo' hakitakutosha!Jirani zangu wawili ambao ni vijana kiumri wana watoto wachanga/wadogo. Wa kwanza aliwahi kuzalishwa na mtoto alipoanza kutembea akampost mkoa kwa babu zake. Yeye anakula raha tu kwa ninavyomwona. Ndio kwanza anasoma ile stail ya 2 in 1 ya sec. Wa pili ni binti yuko chuo kikuu. Ana bwanaake wanaishi wote. Nae anasoma ila sijui wapi. Hawa mtoto wao alipofikisha miezi 3 walimpost kwa bibi hapahapa dar kwa kisingizio cha shule. Malezi ya hawa watoto yanakuwaje? Swali langu ni kuwa kuna ulazima wa kukimbilia kuzaa wakati mambo mengine yamekubana? Tulijadili hili
nakubaliana kabisa na wewe kwenye sual la kuwahi, ila ndo mtoto wa 3 mon umpeleke kwa bibi yake!? i dont agree here!!!...'insurance' tu hiyo. Hata mimi nilijiwahi na mapeema. Ya nini kusubiria umalize madarasa ilhali elimu haina mwisho? Hakikisha last born wako yupo chuo kikuu kabla hujastaafu, otherwise 'kiinua mgongo' hakitakutosha!
ukiona hivi ujue ni mimba ambazo hazikutarajiwa.
kila mtu ana system yake ya malezi na uzazi, kama walikaa chini na kuamua iwe hivyo na wenyewe wapo happy mimi sioni tatizo hata kidogo
kupanga ni kuchagua
mnh,
hata mie napenda watoto,
lakini nimeona dada yangu akilea wake..si kazi ndogo atii
ningependa kuzaa ila mtu akinihakikishia atanisaidia kulea...
hivi hivi sizai ng'oo...unaweza kufa kwa presha walahi!,
hao wanaopeleka kwa bibi waache wale starehe,
hata mie ningefanya hivyo,nile maisha...
nchi za watu hakuna wa kumpelekea mtoto wako..
unahangaikaaaaaaaaaaaaaaaa naye mwenyewe,!
basi tu kwanza mie mwanangu akiwa na mama yangu nitafeel yuko safe...na atapata malezi mazuri kuliko akiwa na housegirl/boy...
ni njia nzuri ya kumkuza mwanao i think...na sio kuepuka rensponsibility...
Roselyne ndiyo maana idadi ya wanandoa wasiotaka watoto hasa katika dunia ya kwanza inazidi kuongezeka na nchi nyingine hadi kufikiria kuweka incentives za kuwalipa wana ndoa michuzi mikali ili waamue kuwa na watoto, lakini pamoja na hizo incentives bado birth rates ni ndogo sana.
Kazi ipo. Kitendo cha kusema uhakikishiwe malezi kwani wewe huwezi toa huduma? Upande mmoja ni wewe kuwa huru na kuwa na mtoto. Upande wa pili ni malezi ya mtoto husika. Kwa nini mwanao akuone mgeni kwake? Kuna raha gani mwanao akuite shangazi? Bado mapenzi ya mama na baba ni bora zaidi. Sio kuwa wazazi wako wanafurahia sana kuwa na mjukuu asie na mpangilio. Wanakustahi tu. NN kasema vyema ila ajue kuwa hata kwenye ridhaa ya ngono kuna bahati mbaya. Pia mkuu NN hizo vibrators na punyeto sio abstinance bali ni ngono mbadala
kweli kabisaa BAK,bado ukiweigh huto tubenefits ambavyo serikali itatoa...
havitacompensate sleep deprivation,depression,and hardwork inayoassociate na ulezi wa mtoto!
siwashangai wana-opt kutokuwa na mtoto jamani,
kuna vitu vingine havinunuliki na pesa atii...
mnh the way i love my bed,hata unipe shiling ngapi nikae macho siwezi mie :yawn::spy:
dont be sooo naive,
its hard kwa dunia ya sasa kwa wazazi kulea watoto wao au kuwa nao 24/7
i mean utafanya kazi saa ngapi na kama ndio unasoma uzeeni,utasoma saa ngapi?
wengi tumelelewa na watu baki,housegirl wameplay part kubwa sana katika malezi yetu kama sio ndugu mama mdogo etc
katika watu wote,wanaofaa kuwa na mwanao,
bibi na babu still ndio best,watakuwa na uchungu na mwanao kushinda hao watu wengine...
hapana yeye ni mkubwa ila ni mgonjwa- Huyo nyaningabu ni mtoto au mkubwa?
Ni vizuri umeliona hilo mapema kuliko kuamua kuzaa tu na mtu ambaye unamuona kabisa kwamba hatakuwa na msaada wowote katika malezi ya mtoto/watoto na baadaye kuanza kujuta kwa makosa uliyoyafanya. Hawakukosea waliotunga methali, "kubeba mimba si kazi, kazi kulea."