Malezi ya leo


Ewaaa...ni cheap labor haswa! Yaani huwaga nawaonea huruma sana. Kwa kiasi kikubwa hawana legal recourse yoyote kwa sababu siyo kwamba eti wanajaza job application, kazi yenyewe haina job description, and they get paid under the table.

My moral convictions don't allow me to partake in this 'wahudumu wa ndani' business. Never ever.
 


Yaani we acha tu NN. Watu wanawanyanyasa hawa Wafanyakazi wa ndani mpaka unasikia huruma ya hali ya juu tena wala siyo wahindi ni Waafrika wenzetu yaani huwa inaniuma sana. Unamuajiri mtu na kumuamini ndani ya nyumba yako na wakati mwingine kumuachia nyumba akiwa mwenyewe lakini hapo hapo unataka kumnyanyasa kupita kiasi! Akikutenda unakuja juu kwamba hawa Wafanyakazi wa ndani ni wabaya lakini ubaya wako huuoni!
 
Watu mbona tuna watoto na hatukuhitaji wala hatuhitaji wahudumu (maids).

inategemeana na umri wa mtoto pia....kama ni mdogo msaidizi ni wa muhimu(kwangu).


watu wanaishi nchi za nje bila ya maids na wanaweza kulea bila wasi wasi.........................hawa wanawezaje hadi sisi tuhitaji maids nafikiri ndo pakuanzia

hao wa ulaya ndio wanawapeleka kwenye hizo daycare mami.....wakirudi wanajichanganya kama NN hapo...

Hakuna Binadamu anayeshindwa kulea mtoto wake, kama mnyama analea, kulinda na kutunza watoto itakuwa binadamu? Tatizo ni mazingira ya nchi yetu na nchi za nje anakoishi NN, Tanzania hapa sidhani kama kuna the so called "Day care" na kama wapo sidhani kama wanachukua mtoto chini ya Miaka Miwili... Kama mama anafanya kazi, definately atahitaji msaidizi wa kubaki na mtoto yeye akiwa kazini.

Pia inategemea muda wa kazi, kwa mfano Mama ni Nurse na anaingia kazini shift ya usiku, atampeleka wapi mtoto?
 
Mtoto wangu nikalelewe na mtu mwingine ,labda naumwa sijiwezi kabisa na nguvu za kulea hazipo ..mungu nisaidie nitimize azima yangu ya kulea wanangu mimi nikisaidiana na baba yao
 

Acha hizo bana. Mbona enzi wakati mimi nakua kazini kwa mama yangu na kazini kwa baba yangu kulikuwa na daycare? Quemu can vouch this for me as we both attended TFNC's daycare.

Nilikuwa nabadilisha daycare kulingana na ratiba za mama na baba. Kama TFNC na UDSM waliweza kuwa na daycare kwa nini sehemu zingine zishindwe....? Oh wait...enzi hizo kulikuwa hakuna ufisadi uliokithiri....that could be the reason
 

Hebu niambie NN, ulipelekwa ukiwa na umri gani?

Sijui kwa kweli... Labda wanaozijua hizo day care watutajie hapa, kuna wamama wengi wangependa kuwapeleka watoto wao huko...
 
Hebu niambie NN, ulipelekwa ukiwa na umri gani?

Sijui kwa kweli... Labda wanaozijua hizo day care watutajie hapa, kuna wamama wengi wangependa kuwapeleka watoto wao huko...

Nilikuwa mdogo sana. Wazazi wangu wote wawili walikuwa ni wafanyakazi. Umri niliopelekwa sikumbuki lakini nakumbuka range ya miaka ya watoto waliokuwa pale....kuanzia waliokuwa wanavaa diaper hadi wale waliokuwa wamekaribia kuanza darasa la kwanza.

Quemu anaweza akawapa mwanga zaidi. Lakini nilipelekwa daycare ya Tanzania Food and Nutrition Centre, pale Ocean road.....
 
mmhhh mie sitaki kwenda kulea mtoto wangu nchi za ulaya...no way....wala sipendi kulea mtoto wangu kizungu,,,hata huko Europe wange pewa hii facility wengi wasingeikataa...

plus its not very cheap to have a maid in my country...na pia kuna sheria za kuajiri, na yote ulio mention hapo....

So i am still keeping my maids.... I need them and they need me...
 
bongo mtu mwenyewe hohe hahe na anamfanyakazi wa ndani!

mfanyakazi wa ndani hajasomea kulea watoto, lakini unamuachia mtoto wako mchanga amlee, na on top unampa na mateso ya kila aina.

hii kitu imenikumbusha novel moja inatwa the Help inayozungumzia namna watu waupe walivyokuwa wakiwanyanyasa watu weusi lakini wakiwaachia wawapikie, wawalelee na watoto wao.

kwetu si watu weupe, ni sisi kwa sisi........
 
sasa hao maids si wanatafuta maisha pia ..nyie msipo waajiri waende wapi?
 
Mwisho wa siku kila mzazi atafanya uamuzi kulingana na kile anachokiona kinafaa kwa mwanae. Watu tumetofautiana malezi ya watoto bana...asikwambie mtu.

Siku moja nilikuwa mall...basi kukawa na katoto flani katundu katundu...kalikuwa kanamkimbia huku na kule. Basi mama yake akakakimbiza na kukapa bonge la kibao. Aisee moyo wangu uliwaka paaaa....nikakaonea huruma sana. Yaani ilibaki kidogo nipige simu Child Protective Services kwa sababu that smacking was way beyond the bounds of moderation.

Personally I don't believe in spanking. I can't spank a child. So when I see one getting spanked it pains me a lot. Ngabu loves the kids man....

Matter of fact, Ngabu Daddy Daycare is coming soon to a neighborhood near you....
 
BAK i am with you...kunyanyasa mtu yeyote si vizuri kabisa...yani unaweza kupata tabu duniani ukiwa hujui kuishi na watu vizuri... hata kama wewe ni CEO wa company ukianza kunyanyasa wafanyakazi wako...unaweza kusababisha company ifungwe....
 
Ufisadi, umalaya, akili ndogo, kutowajibika, kutoheshimu, uvivu, et al ni chimbuko la malezi haya tunayoyasemea. Kwao wote walioenda kinyume na hii mada wangelitamani kipindi cha ujauzito kama kungekuwa na mbadala wa kubeba mimba wangeuchangamkia.
 
BAK i am with you...kunyanyasa mtu yeyote si vizuri kabisa...yani unaweza kupata tabu duniani ukiwa hujui kuishi na watu vizuri... hata kama wewe ni CEO wa company ukianza kunyanyasa wafanyakazi wako...unaweza kusababisha company ifungwe....

Yaani, kuna watu wana roho mbaya jamani! Unamnyanyasa binadamu mwenzako eti kwa vile umemuajiri na unamlipa mshahara.

Binadamu tunatofautiana kusema kweli NN. Niliyowahi kuyaona wakitendewa Wafanyakazi wa ndani Bongo hadi leo hii nikiyakumbuka huwa yananisikitisha sana.
 

sasa huyu mama yangu nae si ana kazi anafanya, ina maana aache shughuli zake ili anilele mtoto? Duu au unaongelea wamama wa nyumbani wasio na kazi, kazi yake ilikuwa kunilea mimi sio na watoto wangu tena, ebu tuwahurumie wazazi wetu, hawajaja duniani kuwa busy na watoto kila cku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…