Mali iliyoko Singida ni utajiri kwa watu wake na Taifa

Mbeya ni zaidi Singida
 
Hapo namba 4 sio Mihama bali Mifama, matunda yake yanaitwa mafama, ndani yana rangi ya njano. Matamu kishenzi[emoji39]
Mihama na mahama ndiyo majina halisi mikoa mingi ya magharibi, kama kwenu inaitwa hivyo nalo ni sahihi, ng'ombe akiitwa ngombe huko Bukoba ni sahihi pia.
 
Sawa nitakuja kwa ajili ya UWEKEZAJI
 
.... ongezea:-
11. Asali (nyuki wakubwa na wadogo).
12. Mbao - MNINGA
13. Tundu Lissu - product ya Singida hii; libarikiwe tumbo lililomzaa.
14. Mifugo
15. Humble people - generally ni watu wasio na tabia za ajabu ajabu.
16. n.k.
Elezea kuhusu asali hapo..! Natamani kujua kwa undani..
 
Elezea kuhusu asali hapo..! Natamani kujua kwa undani..
... sina statistics kamili ila mchango wa Singida kwa asali inayoliwa nchini ni mkubwa sana (along with Tabora).
 
... sina statistics kamili ila mchango wa Singida kwa asali inayoliwa nchini ni mkubwa sana (along with Tabora).
Kule kuna asali nyingi sana hasa wilaya ya manyoni iliyopakana na Tabora asali ni ya kutosha.
Kuna kipindi baada ya kumaliza chuo nilikuwa nafundisha shule za vijijini(tempo) kuna wanafunzi walikuwa wananiletea asali kisado kizima bure wanarina wao wenyewe.
 
...Tatizo nini, halifanyiwi Kazi hili??
 
Singida ni moja ya mikoa maskini sana hapa TZ, licha ya fursa za kiuchumi ulizozitaja.
Angalau kwa sasa mabadiliko yanaanza taratibu.
Tatizo wanyaturu ni wavivu sijapata ona alafu wanapenda kusema wageni wao kwa ubaya tena kwa kilugha aisee ule mkoa sio wa kuishi kabisa ata kidogo
 
Mkuu mazao mengi ulioyataja yanalimwa na mikoa mingine mbeya Njombe,iringa nk yote wanalima vitunguu,alizeti nk.
Kingine singida haina mvua za uhakika kama pwani, kusini na magharibi hivyo mtu atoke songea mbeya,Njombe,Tabora,Mwanza, Moshi, nk aende singida ni ngumu. Ila ni rahisi watu kwenda katavi, nyanda za juu kusini, Moro nk huko uhakika wa mvua na kuvuna.Pambaneni mmeletewa soko karibu ila kutushawishi kuja singida ni ngumu sana.
 
.... ongezea:-
11. Asali (nyuki wakubwa na wadogo).
12. Mbao - MNINGA
13. Tundu Lissu - product ya Singida hii; libarikiwe tumbo lililomzaa.
14. Mifugo
15. Humble people - generally ni watu wasio na tabia za ajabu ajabu.
16. n.k.

Kuna ulazima gani wa kutaja taja hilo jina la huyo mtu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…