Agosti 17, 2026, Mahakama ya Mali imemhukumu kifungo cha miaka saba jela mtangazaji maarufu na influencer wa mitandaoni, ambao wote walikuwa wakikosoa utawala wa kijeshi nchini humo
Mtangazaji wa televisheni na redio, Mohamed Youssouf Bathily, maarufu kama Ras Bath, amehukumiwa na mahakama ya Bamako kwa makosa ya kula njama na kuichafua serikali, pamoja na Rokia Doumbia, influencer anayefahamika mtandaoni kwa jina la “Rose, the cost of living.”
Wawili hao walikuwa wamezuiliwa kwa miaka kadhaa kufuatia kipindi kilichorushwa mwaka 2023 na Ras Bath, kilichozungumzia changamoto za kiuchumi zinazowakabili wananchi wa kawaida nchini Mali.
Ras Bath alikuwa kizuizini tangu Machi 2023. Muonekano wake uliodhoofika na kukonda sana ulizua mshangao miongoni mwa Wamali wengi alipojitokeza mbele ya mahakama wakati kesi yake ilipoanza Agosti 10, 2026 katika Mahakama ya Rufaa ya Bamako.
Waendesha mashtaka walidai kuwa mtangazaji huyo na Doumbia walikuwa wakishirikiana, wakisema Ras Bath alikuwa amemualika “Rose” kwenye kipindi chake mara mbili hapo awali. Hata hivyo, mawakili wa Ras Bath walipinga madai hayo.
Ras Bath alikamatwa kwa mara ya kwanza nchini Mali Agosti 2016 kwa tuhuma za “kuchochea wanajeshi kutotii”, lakini aliachiliwa baada ya siku mbili kutokana na shinikizo kutoka kwa wafuasi wake.
Julai 2017, akiwa nje ya nchi, alihukumiwa bila kuwepo mahakamani kifungo cha miezi 12 jela, ingawa hakuwahi kutumikia kifungo hicho.
Pia alishiriki katika maandamano ya vuguvugu la M5-RFP mwaka 2020 yaliyompinga Rais Ibrahim Boubacar Keita, ambaye baadaye aliondolewa madarakani na maafisa wa jeshi walioahidi kukabiliana na uasi wa muda mrefu wa makundi ya kijihadi nchini humo.
Desemba 2020, mtangazaji huyo alikamatwa tena katika kesi iliyohusisha madai ya njama dhidi ya utawala wa kijeshi. Baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali kwa kukosekana kwa ushahidi, aliachiliwa Aprili 2021.
Julai 2023, aliachiliwa huru katika kesi nyingine ambapo alituhumiwa kutoa madai ya uongo kwamba aliyekuwa Waziri Mkuu, Soumeylou Boubeye Maiga, “aliuawa” akiwa kizuizini chini ya utawala wa kijeshi.
Tangu jeshi lilipochukua madaraka, limeweka vikwazo vikali dhidi ya uhuru nchini Mali, likipunguza nafasi ya sauti za upinzani kupitia matumizi ya mahakama, shinikizo na kuvunjwa kwa vyama vya siasa.
Aliyeshikilia mic, Mohamed Youssouf Bathily, Maarufu Ras Bath
Source: African news