Mali yapendekeza Uchaguzi kucheleweshwa kwa miaka mitano

Mali yapendekeza Uchaguzi kucheleweshwa kwa miaka mitano

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Serikali ya mpito nchini Mali imependekeza kwa majirani zake wa Afrika Magharibi kuahirishwa kwa uchaguzi kwa miaka mitano, baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2020.

Waziri wa Mambo ya Nje Abdoulaye Diop amesema haya katika maoni yaliyotangazwa kupitia kituo kinachoendeshwa na serikali baada ya mkutano na rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS)

Awali serikali ya mpito ilikubali kuandaa uchaguzi wa urais na ubunge mnamo Februari 2022, miezi 18 baada ya Kanali Assimi Goita kuongoza mapinduzi dhidi ya Rais Boubacar Ibrahim Keita.

Tangu wakati huo kumekuwa na maendeleo kidogo katika maandalizi ya uchaguzi huku wakisema kunatokana na mivutano na ghasia kutoka kwa makundi ya wapiganaji wa Kiislamu.

DW Swahili
 
Back
Top Bottom